Ijumaa, 13 Aprili 2018

NAMNA YA KUISHI NA WATU JIFUNZE

Mojawapo ya mambo muhimu katika mafanikio ya aina yoyote maishani ni kupata msaada wa aina Fulani kutoka kwa watu wengine. Mtu hawezi kufanikiwa bila msaada wa watu,kwa maana hakuna mtu anayejua kila kitu/jambo na anayeweza kufanya kila kitu Duniani.

Kwa namna yeyote ile mtu anahitaji msaada wa wengine. Hivyo ili kupata msaada wa wengine ni lazima kujua namna ya kuishi na watu vizuri.Ingawa siyo rahisi kumpendeza kila mtu, lakini watu wengi utaishi nao kwa amani. Zifuatazo ni KANUNI na MBINU mhimu za kuishi na watu vizuri._

_1) Uwe na tabia ya kupenda watu kwa moyo wote,hali kadhalika na wewe watakupenda._

_2) Heshimu kila mtu na kila mtu umwone ni muhimu sana na wa maana._

_3) Usimdharau mtu yeyote kutokana na hali yake,hata akiwa ni masikini ,hakuelimika,hana cheo cha juu na kadhalika._

_4) Uwe mtu wa furaha na tabasamu unapokutana na watu._

_5) Uwe mcheshi na mtu ambaye watu wanafurahi kuwa nawe._

_6) Usipende kulaumu watu na kama utalaumu mtu,tumia njia nzuri na ya upole ya kumsaidia na kumjenga._

_7) Usiwe msengenyaji na usimseme mtu vibaya._

_8) Usipende kugombeza na kutukana au kutoa matusi kwa watu._

_9) Shukru kwa kila jambo jema linapotendeka kwa kusema ahsante au shukru kwa kila jambo._

_10) Usiwe mtu wa kujipendekeza kwa watu au wakubwa._

_11) Usipende mabishano na kama yakitokea,usitake kila mara kushinda._

_12) Uwe mpole na usiwe mkali kwa watu._

_13) Usipende kugombana,kupiga au kupigana na watu._

_14) Uwe mnyenyekevu na usijivune kwa kwa lolote lile,kama kuna jambo zuri kwako acha wengine wakusifu._

_15) Usiwe na kinyongo,fitina na usitunze chuki._

_16) Usilipize kisasi,badala yake tenda wema kwa Yule anayekukosea._

_17) Usiwe unachonganisha watu,ukiambiwa udhaifu wa mtu usiende kumwambia aliyesema._

_18) Jipende na kujikubali kama ulivyo kimaumbile na uwezo wako,ndipo na watu nao watakupenda na kukubali kama ulivyo._

_19) Tunza siri zako na za wengine._

_20) Usiwe mwepesi wa hasira_

_21) Kumbuka majina ya watu unaokutana nao._

_22) Usiwe mzungumzaji kupita kiasi,badala yake uwe msikilizaji mzuri._

_23) Usiseme uongo au kuongeza chumvi au kupotosha ukweli._

_24) Zungumza kufuatana na mambo mtu anayoyapenda._

_25) Maliza ugomvi au migogoro na wengine kwa njia ya amani kwa kuzungumza na mhusika._

_26) Jifunze kusamehe makosa ya watu._

_27) Unapofanya makosa,kubali na kuungama na kuomba msamaha._

_28) Heshimu na kuvumilia mawazo na maoni ya wengine ambayo ni tofauti na yako._

29) Nigongee like hata kama hujaipenda hii. Mia

Mwanamuziki tajiri nchini Tanzania huyo hupa

Jarida la Forbes la nchini marekani limetoa wasanii matajiri zaidi duniani ,Africa na kanda mbali mbali ambapo kwa upande wa Africa mashariki.

Diamond platinum ameongoza kwa kuwa na utajiri wa dollar million 4.5 ambazo ni zaidi ya bilioni 10 za kitanzania hasa baada ya kununua Nyumba yake ya south Africa.

Vitu vingine anavyomiliki ni Majumba ya kifahari Dar,Magari ya kifahari , Berber shop, Maduka ya nguo za mitindo ya kisasa na vingine Vingi.

Amefatiwa na Dr Jose Kamilioni wa Uganda ambaye anakadiliwa kuwa na utajiri wa dollar milioni 3.9 ... Wanafatia Akothee na Jaguar anashika nafasi ya 4

Wanachokiangalia zaidi sio pesa kwenye account Bali thamani ya vitu anavyomiliki.....

Katika jarida hilo linaonyesha diamond akiwa anafanya wastani wa show 2 kwa wiki show 8 kwa mwezi na show 100 kwa mwaka ambapo show yake ya chini anakadiriwa kulipwa wastani wa dollar elfu 20,000 na show ya juu analipwa wastani wa dollar elfu 75,000 .

Mikataba yake na makampuni kama Cocacola,Vodacom na DSTV

Jarida ilo linaonyesha pia diamond anaweza vaa vitu vyenye thamani ya dollar laki 150,000 ambazo ni zaidi ya milioni 350,000,000 za tanzania mwilini mwake kwenye shoo moja ambavyo ni Pete,cheni,viatu kofia,shati na suruali na vingine.

Kiukweli huyu mwenzetu yupo kwenye another level kabisa.

Ongera kwa diamond platinum na wapenda maendeleo wote wa nchi hii tuendelee kumsaport msanii huyu aweze kufika mbali zaidi....   By ZAKABOYBLOG

Jumatano, 11 Aprili 2018

HAUWEZI KUSHINDANA

Hauwezi kushindana, oh kushindana
(You cannot compete, cannot compete)
Na mwanadamu mwenye kinywa
(With a person with a mouth)
(Repeat)
Kama maneno yangekuwa yanaweza kutoboa mwili huu
(If words were able to pierce this body)
Mbona sasa ningekuwa na vidonda mwili mzima
(Then my body would be full of wounds)
Vita vya maneno kuna watu ni majemedari
(In the war of words, there are Generals)
Ukisema mshindane mbona mikono mtainua
(If you were to compete, you will lose)
Kupigwa vita ni kawaida isikusumbue
(Being fought is usual, do not let it bother you)
Wewe ni mti wenye matunda, zoea mawe
(You are a tree with fruits, get used to the stones)
Lia kidogo, nyamaza ili uchungu uishe
(Cry a little, then be quiet that the pain will end)
Ukiendelea unawapa kichwa hao
(When you continue, you confuse them more)
Basi laza imani, rejea vitani
(Then pick up your faith and return to the fight)
Wakikuona waseme, umekuwa sugu
(When they see you to say you have become tough)
Acha waongee, acha waseme seme
(Let them speak, let them talk about you)
Ila yuko Mungu wakuwaziba midomo
(For there is a God that will shut their mouths)
(Refrain)
Ikiwa Mungu anahukumu kwa kusikiza maneno
(If God judged by listening to words)
Mbona hata matumbo ya mimba yanasemwa sana
(Then what of pregnancies that are talked about a lot)
Hivi Mungu angehukumu kwa kusikiza umbea
(If God judged by listening to gossip)
Si ningekushauri mchungaji wangu ufunge kanisa
(Then I would advise you my minister to close the church)
Mwanadamu, mwanadamu shida ni ulimi
(The human, the man has an issue with the tongue)
Ungejifunza ukimya, haunanga hasara
(If you teach it silence, you will not lose)
Fulani, we fulani una shida gani?
(My friend, what is your problem?)
Na uongo wanini? Mwogope Mungu
(Why lie? Fear God)
Ukumbuke ni ahadi, kuna siku yaja
(Remember it is  a promise, that a day is coming)
Kwa kila neno na kinywa chako utatolea hesabu
(That every word from your mouth with be brought to account)
Mimi nimeshakwambia kubali uwache
(I have already told you, agree to leave it alone)
Utajijua na shingo yako ngumu
(You will understand yourself to be tough)
Siwezi kushindana, oh kushindana
(I cannot compete, cannot compete)
Na mwanadamu mwenye kinywa
(With a human with a mouth)
(Refrain)
Yesu, huyu Yesu hakujitetea kabisa
(Jesus, this Jesus did not defend himself)
Japo walimsema kwa ubaya aliwasamehe
(Though they talked with evil intents, He forgave them)
Na wewe uwasamehe, uwaombee
(And you forgive them, and pray for them)
Kwa maana hawayajui wasemaya
(For they do not know ..?)
Wakifingyanga ubaya, uwajibu kwa wema
(When they do wrong, answer them with kindness)
Usishindane na mtu, wajibu kwa wema
(Do not compete with anyone, answer them with kindness)
Ata iwe ni ndugu wa karibu, wajibu kwa wema
(Even if it is your close brother, answer them with kindness)
Si vizuri wewe, usilipe kisasi, wajibu kwa wema
(It is not good for you to revenge, answer them with kindness)
Tena wema uende, wajibu kwa wema
(Do good and leave, answer them with kindness)
Eh, wajibu kwa wema
(Oh, you answer with goodness)
Maana x2
(Because, because)
(Refrain)

JE CHUKI NI NINI ENDELEA HAPA..….!?

by Zakaboy blog
1.Chuki ikikujaa moyoni itakufanya uone kila kitu kibaya na utakua negative zaidi, hata kama kitu kina mazuri yake utapinga hata kwa makusudi ilimradi useme mabaya yake tu

2. Utapata presha na kihoro kwajili hata ya mambo ya kawaida na yasiyokuhusu.

3.Utajikuta unafanya vitu vibaya ambavyo utajutia sana, sababu utafanya ili ujifurahishe wewe, jiulize ukimuumiza mtu asiye na hatia makusudi were utapata nini ukimuona bado anaendelea kuishi kwa amani? si utatamani na uhai wake?!

4.Chuki hupandikiza na hupandikizwa hakuna mtu anazaliwa na chuki, jiepushe na mitazamo has I na kufuata mkumbo.

5.Hakuna jambo hutatuliwa kwa chuki ila upendo, maranyingi watu wenye chuki au kutaka kutatua tatizo kwa chuki maranyingi hukosa maarifa hivyo kuishia kufeli sababu chuki hupumbazwa na hasira, ukipanda ulingoni na hasira utapigwa tu.

6.Chuki binafsi huleta umasikini na watu wachuki binafsi hawanaga maendeleo. Jirani yako alokuzidi akinunua gari usichukie bali hamasika, chukia hali yako ya umaskini ili ufanye kazi kwa bidii utoke kimaisha na ukijichukia mwenyewe hapo umefeli mazima.

7.Chuki huleta wivu, uchawi, masimango, vinyongo, ubaguzi, utumwa wa fikra, chuki ni mateso ambayo huanza na we we mwenyewe

8.Chuki itakuzeesha, itakukondesha, wewe ni shabiki na unamchukia staa ambae hujawahi hata kumuona na hakujui, yeye na matatizo yake akilia analia na Mungu wake wewe, wewe una matatizo yako, unaongeza ya maishan yake sumu.

9.Chuki ni sumu mwilini unaouchosha mwili kwa (stress), chuki nzuri ni ya kimaendeleo chuki nzuri ni ya kuwa na kiu ya kuinua hali ya maisha yako.

Ijumaa, 30 Machi 2018

KWA NINI YESU ALIKUFA

Yesu alikufa ili wanadamu wasamehewe dhambi zao na kupokea uzima wa milele. (Waroma 6:23; Waefeso 1:7) Pia kifo cha Yesu kilithibitisha kwamba wanadamu wanaweza kuendelea kuwa washikamanifu kwa Mungu hata wanapokabili majaribu makali sana.​—Waebrania 4:​15.
Fikiria jinsi kifo cha mtu mmoja kingeweza kutimiza mambo mengi hivyo.
  1. Yesu alikufa ili ‘tusamehewe dhambi zetu.’​—Wakolosai 1:​14.
    Mwanadamu wa kwanza, Adamu, aliumbwa akiwa mkamilifu, bila dhambi. Hata hivyo, alichagua kumwasi Mungu. Adamu alipokosa kutii, au alipotenda dhambi, aliwaathiri vibaya wazao wake wote. Biblia inasema: “Kupitia kutotii kwa mtu mmoja wengi walifanywa watenda-dhambi.”​—Waroma 5:19.
    Yesu alikuwa mkamilifu kama Adamu, lakini yeye hakuwahi kutenda dhambi. Hivyo, yeye angeweza kuwa “dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu.” (1 Yohana 2:2) Kama tu kutotii kwa Adamu kulivyoichafua familia ya wanadamu kwa dhambi, ndivyo kifo cha Yesu kilivyofuta doa hilo la dhambi kutoka kwa wote wanaodhihirisha imani kwake.
    Kwa njia fulani, Adamu aliiuza jamii ya wanadamu katika dhambi. Yesu alipokufa kwa hiari kwa ajili yetu, aliwanunua wanadamu wawe wake. Kwa sababu hiyo, “yeyote akitenda dhambi, tuna msaidizi kwa Baba, Yesu Kristo, mtu mwadilifu.”​—1 Yohana 2:1.
  2. Yesu alikufa “ili kila mtu anayemwamini asiangamizwe bali awe na uzima wa milele.”​—Yohana 3:​16.
    Ingawa Adamu aliumbwa aishi milele, dhambi yake ilimletea hukumu ya kifo. Kupitia kwa Adamu, “dhambi iliingia katika ulimwengu na kifo kupitia dhambi, na hivyo kifo kikaenea kwa watu wote kwa sababu wote walikuwa wamefanya dhambi.”​—Waroma 5:12.
    Tofauti na hilo, mbali tu na kuondoa doa la dhambi, kifo cha Yesu kilifuta hukumu ya kifo kwa wote wanaodhihirisha imani kumwelekea. Biblia inakazia jambo hilo kwa njia hii: “Kama vile dhambi ilivyotawala kama mfalme pamoja na kifo, vivyo hivyo pia fadhili zisizostahiliwa zitawale kama mfalme kupitia uadilifu kwa tazamio la uzima wa milele kupitia Yesu Kristo Bwana wetu.”​—Waroma 5:​21.
    Bila shaka, wanadamu leo wanaishi kwa muda mfupi sana. Hata hivyo, Mungu anaahidi kwamba atawapa wanadamu waadilifu uzima wa milele na kufufua wafu ili wao pia wafaidike kutokana na dhabihu ya kifo cha Yesu.​—Zaburi 37:29; 1 Wakorintho 15:22.
  3. Yesu ‘alikuwa mtiifu mpaka kifo,’ na hivyo kuthibitisha kwamba mwanadamu anaweza kuwa mwaminifu kwa Mungu anapokabili jaribu lolote.​—Wafilipi 2:8.
    Licha ya kuwa na akili na mwili mkamilifu, Adamu alimwasi Mungu kwa sababu kwa ubinafsi alitamani kitu ambacho hakikuwa mali yake. (Mwanzo 2:​16, 17; 3:6) Baadaye, Shetani, adui mkuu wa Mungu, akadai kwamba hakuna mwanadamu anayeweza kumtii Mungu bila ubinafsi, hasa ikiwa uhai wake uko hatarini. (Ayubu 2:4) Hata hivyo, mwanadamu mkamilifu Yesu alimtii Mungu na kudumisha ushikamanifu kwake, hata akakabili kifo kinachofedhehesha na kilicho na maumivu. (Waebrania 7:​26) Suala hilo lilitatuliwa kikamili: Mwanadamu anaweza kudumisha uaminifu wake kwa Mungu anapokabili jaribu lolote lile.
Yesu akiwa kwenye mti wa mateso katikati ya wezi wawili

Maswali kuhusu kifo cha Yesu

  • Kwa nini Yesu alilazimika kuteseka na kufa ili kuwakomboa wanadamu? Kwa nini Mungu hakufuta tu hukumu ya kifo?
    Sheria ya Mungu inasema kwamba “mshahara ambao dhambi hulipa ni kifo.” (Waroma 6:23) Badala ya kumficha Adamu sheria hii, Mungu alimwambia kwamba hukumu ya kutotii ni kifo. (Mwanzo 3:3) Adamu alipofanya dhambi, yule Mungu “asiyeweza kusema uwongo,” alitimiza alichokuwa amesema. (Tito 1:2) Kwa hiyo, Adamu hakuwapitishia wazao wake dhambi tu, bali pia aliwapitishia malipo ya dhambi, yaani, kifo.
    Ingawa wanadamu wenye dhambi wanastahili adhabu ya kifo, Mungu aliwapa “utajiri wa fadhili zake zisizostahiliwa.” (Waefeso 1:7) Uandalizi wake wa kuwakomboa wanadamu, yaani, kumtuma Yesu awe dhabihu kamilifu, ulikuwa uandalizi wa haki na wenye rehema nyingi.
  • Yesu alikufa lini?
    Yesu alikufa “saa tisa” alasiri siku ya Pasaka ya Wayahudi, yaani, saa ya tisa tangu mapambazuko. (Marko 15:33-​37.) Tarehe hiyo inalingana na Ijumaa, Aprili 1, 33 W.K., kulingana na kalenda za kisasa.
  • Yesu alifia wapi?
    Yesu aliuawa mahali “panapoitwa Mahali pa Fuvu la Kichwa, panapoitwa Golgotha katika Kiebrania.” (Yohana 19:17, 18) Katika siku za Yesu, eneo hilo lilikuwa “nje ya lango” la Yerusalemu. (Waebrania 13:12) Huenda lilikuwa kwenye kilima, kwa kuwa Biblia inasema kwamba wengine walitazama kuuawa kwa Yesu “wakiwa mbali.” (Marko 15:40) Hata hivyo, leo eneo la Golgotha haliwezi kusemwa kihalisi lilikuwa wapi.
  • Yesu alikufa jinsi gani?
    Ingawa watu wengi wanaamini kwamba Yesu alisulubiwa, yaani, aliuawa kwenye msalaba, Biblia inasema hivi: “Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti.” (1 Petro 2:​24Union Version) Waandikaji wa Biblia walitumia maneno mawili ya Kigiriki kurejelea vifaa vilivyotumika katika kifo cha Yesu​—stau·rosʹ na xyʹlon. Wasomi wengi wamefikia mkataa kwamba maneno hayo yanawakilisha nguzo au mti ulionyooka na kufanyizwa kwa kipande kimoja tu cha mbao.
  • Kifo cha Yesu kinapaswa kukumbukwa jinsi gani?
    Usiku wa Pasaka ya kila mwaka ya Kiyahudi, Yesu alianzisha mwadhimisho usiohusisha mambo mengi akiwa na wafuasi wake na kuwaamuru hivi: “Endeleeni kufanya hivi kwa kunikumbuka mimi.” (1 Wakorintho 11:24) Saa kadhaa baadaye, Yesu aliuawa.
    Waandikaji wa Biblia walimlinganisha Yesu na mwana-kondoo aliyetolewa dhabihu siku ya Pasaka. (1 Wakorintho 5:7) Kama tu mwadhimisho wa Pasaka ulivyowakumbusha Waisraeli kwamba walikuwa wamekombolewa kutoka utumwani, vivyo hivyo Ukumbusho wa kifo cha Yesu Kristo unawakumbusha Wakristo kwamba wamekombolewa kutoka katika dhambi na kifo. Pasaka ilikuwa sherehe iliyofanywa mara moja kwa mwaka, siku ya Nisani 14 kulingana na kalenda ya Kiyahudi; vivyo hivyo Wakristo wa mapema walifanya Ukumbusho mara moja kila mwaka.
    Kila mwaka, kwenye tarehe inayolingana na Nisani 14, mamilioni ya watu ulimwenguni pote wanaadhimisha kifo cha Yesu.

Ijumaa, 23 Machi 2018

JUA FAIDA ZA KUCHEKA NA KUTABASAMU




Kama wengi wetu tujuavyo, kiwango cha miaka ya kuishi hasa katika nchi za ulimwengu wa tatu kimepungua sana nyakati hizi, hivyo kila tunaposherekea mwaka mpya tunasherekea pia uzee na utimilifu wa miaka yetu ya kufa, lakini hilo lisitupe hofu kwani wataalam wamegundua maajabu yapatikanayo kwa mtu kucheka.

Kwa kutambua umuhimu wa maajabu hayo nimeona ni vema nikaelezea faida za mtu kucheka. Ifahamike kuwa watafiti mbalimbali duniani wamebaini kuwa mtu anaweza kujikinga, kujiponya na magonjwa hatari ya kansa, moyo na kisukari kwa kucheka na isitoshe achekaye anatajwa kuufanya mwili wake usionekane umezeeka hata kama atakuwa na umri mkubwa.


Kwa mujibu wa watafiti wa masuala ya kijamii, ugumu wa maisha unaoleta msongo wa mawazo ndiyo unaotajwa kuchangia vifo vya wanadamu wengi sambamba na kufupisha umri wa kuishi. Wanasema mtu mwenye kutingwa na sononi kila mara huchoma seli nyingi muhimu katika mwili wake, hivyo kumfanya awe katika hatari ya kushambuliwa na magonjwa niliyoyataja hapo juu.

Katika tafiti za hivi karibuni ukiwemo ule uliyoendeshwa na wasomi wa Chuo Kikuu cha Amerika Cardiology, imebainika kuwa uhaba wa furaha hasa fursa ya watu kupata muda wa kucheka kwa siku ni moja kati ya sababu kubwa zinazochangia magonjwa hatari miongoni mwa watu wengi. Wanasema watu wengi wamechipusha vimelea vya magonjwa si kutokana na bakteria halisi bali mfadhaiko wa mioyo yao.

Kwa maana hiyo wataalam hao wameibuka na ushauri kuwa ni bora watu wakajibidisha kutafuta furaha katika maisha yao kuliko kudumu katika uhangaikia tiba ghali za dawa zinazotolewa na vituo vya afya na hospitali, ilhali mzizi wa magonjwa yao unatokana na wao wenyewe kuishi bila kicheko ambacho kinatafsiri furaha aliyonayo mtu husika (kumbuka sizungumzii kicheko cha kebehi).

Kwa mujibu wa wasomi hao imegundulika kuwa kicheko ni tiba na kinga bora ya magonjwa yanayomkabili mwanadamu yakiwemo magonjwa ya moyo ambayo ni hatari sana kwa uhai. Mtu ambaye anaweza kutumia dakika 20 kwa siku kwa kucheka, anaweza kutibu maradhi yake hata bila kumeza vidonge.
By zakaboyblog.blogspot.com

Jumatano, 21 Machi 2018

JE NI NINI KUWAHESHIMU BABA NA MAMA....?

Je ni nini maana ya kuwaheshimu baba yangu na mama?


Swali: "Je ni nini maana ya kuwaheshimu baba yangu na mama?"

Jibu: Kuwaheshimu baba yako na mama ni kuwa wa heshima katika usemi na tendo na kuwa na nia ya ndani ya heshima kwa hali yao. Neno la Kigiriki kwa heshima linamaanisha "stahi, tuzo, na thamani." Heshima haileti sifa tu bali hata cheo. Kwa mfano, baadhi ya Wamarekani wanaweza kutokubaliana na maamuzi ya Raisi, lakini wao bado wanapaswa kuheshimu nafasi yake kama kiongozi wa nchi yao. Vile vile, watoto wa umri wote wanapaswa kuwa heshima kwa wazazi wao, bila kujali kama wazazi wao "wanastahili" heshima au hawastahili.

Mungu Anatusihi tuheshimu baba na mama. Anathamini kuwaheshimu wazazi sana hadi akaijumlisha katika amri kumi (Kutoka 20:12) na tena katika Agano Jipya: "Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii nidyo amri ya kwanza yenye ahadi, Upate heri ukae siku nyingi katika dunia" (Waefeso 6:1-3). Kuwaheshimu wazazi ndio amri pekee katika maandiko inayoahidi maisha ya muda mrefu kama malipo. Wale ambao uheshimuwazazi wao wana heri (Yeremia 35:18-19). Kwa upande mwingine, wale walio na " akili potofu " na wale ambao huonyesha uasi katika siku za mwisho wanatambulika kwa kutotii wazazi (Warumi 1:30, 2 Timotheo 3:2).

Sulemani, mtu mwenye hekima, alitoa wito kwa watoto kuwatii wazazi wao (Mithali 1:8; 13:1; 30:17). Ingawa sisi huenda tusiwe chini ya mamlaka yao tena, hatuwezi kuiondoa ile tabia ya amri ya Mungu kwa heshima ya wazazi wetu. Hata Yesu, Mungu Mwana alinyenyekea kwa wazazi wake wa mwili hapa duniani (Luka 2:51) na kwa Baba yake wa mbinguni (Mathayo 26:39). Kufuatia mfano wa Kristo, tunapaswa tuwachukulie wazazi wetu kwa njia tunayomweshimu Baba yetu wa mbinguni (Waebrania 12:9, Malaki 1:6).

Ni wazi, kuwa tumeamrishwa kuwaheshimu wazazi wetu, lakini jinsi gani? Kuwaheshimu kwa vitendo na tabia (Marko 7:6). Heshimu matarijio yao yaliyotajwa na yale hayajatajwa. "Mwana wa hekima husikiliza mahusia ya baba yake; bali mwenye dharau hasikilizi maonyo" (Mithali 13:1). Katika Mathayo 15:3-9 Yesu aliwakumbusha Mafarisayo amri ya Mungu ya kuheshimu ya baba na mama. Walikuwa wanatii barua ya sheria, lakini wao walikuwa wameiongeza mila zao wenyewe ambazo ziliifutilia mbali amri ya Mungu. Wakati waliheshimu wazazi wao katika neno, matendo yao yalidhihirisha nia yao halisi. Heshima ni zaidi ya huduma ya mdomo. Neno "heshima" katika kifungu hiki ni kitenzi, na kwa hivyo linanahitaji hatua za haki.

Tunapaswa kutafuta kuwaheshimu wazazi wetu njia ile ile sisi hujitahidi kuleta utukufu kwa Mungu-katika mawazo yetu, maneno na matendo. Kwa mtoto mdogo, kutii wazazi huenda sako kwa bako na kuwaheshimu. Hiyo ni pamoja na kusikiliza, kuzingatia na kunyenyekea kwa mamlaka yao. Baada ya watoto kukomaa, utiifu waliojifunza wakiwa watoto utawahudumia vizuri katika kuheshimu mamlaka mengine kama vile serikali, polisi, na waajiri.

Huku tukihitajika kuwaheshimu wazazi,hiyo haijumulishi kuiga wale waovu (Ezekiel 20:18-19). Kama mzazi milele humfundisha mtoto kufanya kitu ambacho ni kinyume na amri za Mungu, huyo mtoto lazima amtii Mungu kuliko wazazi wake (Matendo 5:28).

Heshima huleta heshima. Mungu hawezi heshima wale ambao hawatii amri yake wala kuheshimu wazazi wao. Kama tunatamani kumpendeza Mungu na kuwa na heri, tunapaswa kuheshimu wazazi wetu. Kuheshimu sio rahisi, daima si furaha, na kwa hakika si rahisi kwa nguvu zetu wenyewe. Lakini heshima ni njia fulani kwa lengo letu katika maisha kumtukuza Mungu. "Watoto, watiini wazazi wenu katika kila kitu, maana hiyo humpendeza Bwana" (Wakolosai 3:20).

By zakaboyblog.blogspot.com

Jumatatu, 19 Machi 2018

DIAMOND AMEMJIBU JULIANA SHONZA JIPU

DIAMOND AMJIBU JULIANA SHONZA
 by ZAKABOYBLOG.blogspot.com

"Nipo tayari kufa au kwenda jela kwa Ajili ya BongoFleva
Inawezekana unanizdi Elimu,Cheo Lakini Katika Sanaa Haunizidi hata robo
Sio kukurupuka Kufungia wasanii bila kufanya Research pia hakuna chochote mnachotusaidia mnaonekana kwenye kufungia tu kutoa vitu vitakavyotujenga wasanii hakuna"
#Diamond_In_TimesFm
By zakaboyblog.blogspot.com

SAMATTA WASILI UWANJA WA NDEGE KURUD TZ

                  zakaboyblog.blogspot.com
Mshambuliaji Mtanzania, Mbwana Ally Samatta, amewasili leo katika Uwanja wa Ndege wa Algiers, Algeria, na kupokelewa na Balozi wa Tanzania nchini humo, Omar Yusuph Mzee.

Samatta amewasili Algeria kwa ajili ya mchezo wa kirafiki, ambapo Taifa Stars itacheza dhidi ya Algeria, Machi 22 2018.

Mchezaji huyo ataungana wa wenzake wa Taifa Stars, walioondoka leo nchini kuelekea Algeria kushiriki mechi hiyo ya kirafiki. 
By zakaboyblog.blogspot.com
JINSI YA KUMSHUGULIKIA MTU AKUSEMAYE VIBAYA AU MWENYE ROHO MBAYA



Mtu mwenye Roho mbaya ana majina mengi na ana nazo sifa nyingi zinazo mtambulisha na wanapatikana katika kila nyanja ya maisha. Toka kwa Mtoto mdogo hadi mkongwe ,Msomi na hata asiye msomi  muumini wa Dini na kwa wapagani pia.Wao sifa zao kubwa ni kuzungumza ya watu na kulaumu wengine kuwa wana makosa. Watu wa jinsi hupenda kuua ujasiri wako kwa kukulaumu hata kwa matendo ambayo hukufanya au umefanya lakini ilikuwa sio kwa nia mbaya.Hupenda kubadili habari njema yako kuwa mbaya hubadilisha  mtazamo wako .Mara nyingi husababisha wewe uwe na msongo wa Mawazo na Afya Mbaya.watu wa jinsi hii huyafanya maisha yako kuwa ya Mashaka na upweke.Masengenyo  yao na ubaya wao huusambaza ili maisha yako yaharibikiwe na uonekane duni katika jamii na Ndugu zako.
Kuwa shughulikia watu wa jinsi hii huwa ni ngumu na hasa wale wenye tabia ya kulaumu na kusambaza lawama kwa Jamii .Ndugu na rafiki zako.Mara nyingi jambo baya likitokea katika jamii mara nyingi kulielekeza kwa wengine iliwao wasionekane wabaya kwa kukusukumia lawama.Kuwashughulikia watu wa Jinsi hii mara nyingi hukuacha uwe na Msongo wa mawazo na kuwa na Afya mbaya .Ushauri mzuri ni kuwapuuza na kuwatoa katika mzunguko wa maisha yako.Sio rahisi kuwatambua watu wenye tabia mbaya kirahisi kwakuwa wanakuja katika kila aina ya Maisha ya Binadamu.Nita kwenda kujadili sifa chache ambazo zita mtambulisha mtu mwenye Roho mbaya na Baadae nitatoa njia ya jinsi ya Kuepukana nao .

SIFA ZA DALILI ZA MTU MBAYA
1Mtu mbaya huwa hakubali kuwa amefanya kosa hata kama amekosea atatafuta njia ya kuipeleka lawama kwa mwingine au atatengeneza kila njia kuhakikisha anamkoseha mwingine kwa kumshauri vibaya au kumshawishi atende jambo baya ililile kosa alilofanya yeye lihamie kwa mwingine aionekane yeye kuwa amehusika na kosa hilo.Na hawa ombi msamaha kokote kwakuwa wao wanajiona kuwa hawana hatia.
Na hata wakiomba msamaha huwa ni wa kinafiki bado wakikurudishia lawama kwako kwamba kama usingelikuwa wewe wasingalikosea hivyo ni kwa makosa yako ndiyo maana wamekosea.Mara nyingi watu kama hawa  hupata sifa yakufanya vizuri kama tatizo likiisha vizuri na wewe kuonekana kama hufai mbele za wengine yeye akiwa ana faa zaidi yako.
2.Mtu mbaya kukataa hata kama amefanya kitu kibaya hakubaki kuwa amekifanya yeye hata kama unaushahidi wa kutosha atakataa na aatsema kuwa wewe ni mwongo atabisha kwa kuwa watu kama hao huwa hawayakubali makosa  yao.Hata kama wanajua kuwa wamekosea mtu mbaya atendelea kubisha tu iliaonekane kuwa hana hatia hata kama anayo hatia ya kosa alilolifanya na ushahidi upo lakini ataendelea kubisha na kutafuta namna ambayo aonekane ni mwema na wewe ni mbaya.
3Mtu muovu hushangilia na kuyatangaza mambo yako kwa wengine haraka sana anapokugundua umefanya makosa .sababu kubwa ili yeye aonekane kuwa ni mwema kwa jamii na ndugu wewe ni mbaya sana .Watu wabaya hujitahidi sana kukupiga majungu iliusifanikiwe na hasa wakiona umepata fursa ambayo wao pia wanaweza kuipata hujitahidi sana kutapakaza uvumi wa uongo haraka sana iliiwezekusikika na kwa uovu wao wata kusema vibaya ili ukate taama usifanikishe katika fursa iliyojitokeza ili wao waichukue fursa hiyo.
4Bahati mbaya sana watu wabaya huwa  hawajitambui kuwa ni wa baya kiasi gani.Na huwa hawa sikii maumivu au hisia ya uchungu wanayokufanyia.Na hata wakijua kuwa umetambua uovu wao watakuambia nilikuwa na kutania tu maana wao wema kwao kumetiwa ganzi na wanafurahia kukuumiza kwa maneno au kwa maandishi yao.Hufurahi kukukebehi wakiwa wanajua kuwa wana kuumiza wao  haiingii Akilini mwao kuwa wanatenda lakukuumiza kwakuwa wanafurahia kuumia kwako..
5Watu wabaya Wanaamini kuwa mahitaji yao ni ya muhimu kuliko yako.Matakwa yao na mahitaji yao ni ya muhimu kuliko yako.Hupenda sana kuutumia mgongo wako kuficha uovu wao iliwao wapate na wewe ubebe lawama zao.
6.Tabia nyingine mbaya ya watu hao ukijihami kutokana na tamia mbaya yao watakuzulia jambo na kulitangaza vibaya iliuonekane wewe ni mbay
By zakaboyblog.blogspot.com

Jumamosi, 17 Machi 2018

ZIFAHAMU ALAMA ZA MYAMA NA. MAANA ZAKE HAPA


By zakaboyblog.blogspot.com
IFAHAMU CHAPA YA MNYAMA NA SANAMU YAKE;
Somo hili ni mwendelezo wa somo linalosema chimbuko la Taifa la Marekani
YAFUATAYO NI MAMBO TUNAYOJIFUNZA HAPA
I. MNYAMA ANAWAKILISHA - Ufalme au Taifa
UFUNUO 7:17 Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea Duniani.
II. MNYAMA ATAKAVYONENA KAMA JOKA
Mnyama mwenye pembe mbili - Huwakilisha Taifa la Marekani
UFUNUO 13:11-14 Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka. Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona. Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu.Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi. MAELEZO YA ZIADA
KATIKA KITABU CHA TUMAINI KUU SURA 25,UK 275
Pembe kama za mwanakondoo na sauti ya joka vinaonesha ukinzani utabiri kwamba ATANENA “KAMA JOKA na kutumia nguvu zote za yule mnyama wa kwanza unaonesha roho ya kutokuvumiliana na mateso ya yule joka na yule mnyama aliye mfano wa chui. na ule usemi kwamba yule mnyama mwenye pembe mbili AIFANYA DUNIA NA WOTE WAKAAO NDANI YAKE WAMSUJUDIE MNYAMA WA KWANZA .unaonesha kwamba mamlaka ya Taifa hili italazimisha utii kwa mamlaka ya PAPA
Kitendo kama hicho kitakuwa kinakinzana na mfumo wake wa taasisi huru .Tamko la uhuru na katiba inasema Bunge halitatunga sheria inayopendelea taasisi ya kidini au kuzuia uhuru wa kidini na kwamba hakuna sharti la kidini litakalozingatiwa kama sifa ya kuchaguliwa kushika ofisi yoyote ya serikali iliyo Nchini Marekani katika kielelezo hiki KUMEONENYESHWA UVUNJAJI WA MAKUNDI WA MIHIMILI HII YA UHURU.Mnyama mwenye pembe kama za mwana kondoo ambaye kwa maneno ni msafi,mpole na siye na madhara –ATANENA KAMA JOKA
III. NJISI SANAMU YA MNYAMA ITAKAVYOUNDWA
ILI MAREKANI IUNDE SANAMU YA MNYAMA ni lazima mamlaka za kidini zidhibiti utawala wa kiraia kiasi kwamba serikali itatumiwa pia na kanisa kutimiza makusudi ya kanisa
Tofauti kubwa ya imani katika makanisa ya KIPROTESTANTi inachukuliwa kama ushahidi kwamba hakutakuwa na mwafaka wa lazima.lakini kwa miaka kadhaa kumekuwa na mwelekeo miongoni mwa MAKANISA YA KIPROTESTANTI wa kutaka mwungano.ili kuwa na mwungano wa aina hiyo ,MIJADALA YA MAMBO AMBAYO WOTE WALIKUWA HAWAKUBARIANI ITABIDI IWEKWE KANDO. katika juhudi za kufikia mwafaka kamili , itakuwa imebaki kidogo tu kugeukia matumizi ya nguvu
MAKANISA MAKUBWA YA MAREKANI yakiwa yameungana katika masuala ya mafundisho yanayoshikwa na wote ,yatakapoishawishi serikali kulazimisha imani zao na kuunga mkono taasisi zao,MAREKANI YA KIPROTESTANTI itakuwa IMEUNDA SANAMU YA UTAWALA WA KANISA LA ROMA na taabu ya adhabu za kiserikali kwa wanaopinga itafuata bila shaka
IV. KUTIA PUMZI KATIKA ILE SANAMU YA MNYAMA
UFUNUO 13 :15
Akapewa kutia pumzi ka tika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. MAELEZO YA ZIADA
KITABU CHA TUMAINI KUU SURA YA 25,UK 279
Waandishi wa kikatoliki huelezea badiliko hilo kama ishara ya mamalaka ya kanisa Katoliki wakisema kitendo cha KUIBADILI SABATO kwenda JUMAPILI ,jambo ambalo WAPROTESTANTI wanaliafiki......kwani kwa kushika jumapili ,wanakiri uwezo wa kanisa kuweka sikukuu na kuamuru zishikwe CHINI YA DHAMBI
Sasa badiliko la sabato nini? kama siyo ishara au alama ya mamalaka ya kanisa la Rumi –Alama ya manyama ? kanisa la Roma halijakanusha madai yake ya ukuu .ulimwengu pamoja na makanisa ya KIPROTESTANTI wanapoafiki sabato iliyowekwa na kanisa hilo huku wakiikataa sabato ya biblia kimsingi wanakubaliana na madai hayo kwa kufanya hivyo wanaipuuza kanuni ambayo inawatofautisha na kanisa la Roma isemayo biblia ,biblia pekee ndiyo dini ya waprotestanti kadiri harakati za kulazimisha
 By zakaboyblog.blogspot.com

YANGA IMEONDOLEWA RASMI KWENYE LIGI YA MABINGWA AFARIKI NA HIZI NDIZO SABABU ZA KUONDOLEWA

By zakaboyblog.blogspot.com
Yanga imeondolewa rasmi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia suluhu ya 0-0 dhidi ya Township Rollers jioni hii.

Township Rollers wamefanikiwa kusonga mbele mpaka hatua ya makundi, baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Dar es Salaam, kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Kazi nzuri waliyoifanya Township kwenye mechi ya awali, inawafanya Yanga kuyaaga rasmi mashindano hayo na kuwafanya waangukie Kombe la Shirikisho Afrika ambalo Simba anashiriki.

Baadaye Simba SC nayo itakuwa ina kibarua kuanzia majira ya saa  2 na nusu usiku, kukipiga dhidi ya Al Masry huko mjini Port Said, Misri.

AMRI KUMI ZA MUNGU HIZI HAPA


AMRI KUMI ZA MUNGU

Leo ni jumapili nimeamka na nimeona afadhali nimkumbuke mungu kwa kuzikumbuka hizi amri.

1. Usiwe na miungu mingine ila mimi.

2. Usijifanyie sanamu ya kuchongo.

3. Usilitaje bure jina la BWANA , Mungu wako.

4. Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.

5. Waheshimu baba yako na mama yako upate heri na miaka mingi duniani

6. Usiue

7. Usizini

8. Usiibe

9. Usimshuhudie jirani yako uongo

10. Usitamani chochote alicho nacho jirani yako.

Je? Kwa mtazamo wako hizi amri zinatekelezwa kweli?

Jumatano, 7 Machi 2018

MUNGU HATANIWI SOMA HISTORI HIZI UONE KAMA MUNGU HATANIWI


1. Mtengenazaji meli ya titanic.
Baada ya kutengeneza meli ya TITANIC, mwandishi wa habari alimuuliza ni kiasi gani ilikuwa salama, nae akajibu " Ni salama sana na haiwezi kuzama na hata mungu hawezi kuizamisha".
Nafikiri unajua kilichotokea kuhusu TITANIC

2.AZUZA (mwanamuziki brazil)
Alipokuwa kwenye show yake ndani ya jiji la Rio dejeneiro , alichukua sigara akaanza kuvuta, akachukua nyingine kisha akairusha juu na kusema " Mungu na hiyo yako , chukua na wewe uvute. Alifariki akiwa na miaka 32 kwa ugonjwa wa kansa ya mapafu, ambayo iliharibu sana mapafu yake kuliko mgonjwa yeyote.

3.Christina hewt (mwandishi)
Huyu alikaririwa akisema " Nimesoma vitabu vyote duniani, ila hakuna kitabu kibaya kama biblia, siku chache baada ya kusema maneno hay, mwili wake ulikutwa umeunguzwa moto ambao haijajulikana hadi Leo umesababishwa na nini.

4. John Lennon (muimbaji)
Wakati alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari la gazeti la america alinukuliwa akisema " ukristo utakufa na kutoweka duniani, siwezi kuwa na wasiwas na hilo kwa kuwa Nina uhakika nalo. Huyu naye baada ya mda alikutwa amekufa nyumbani kwake

5. Tancredo neves (rais wa brazil)
Alisema kwamba endapo angeshinda kura laki tano katika uchaguzi mkuu Brazil na kuwa rais , hata mungu asingeweza kumtoa katika urais huo. Akafanikiwa akapata kura zaidi ya laki tano akashinda uchaguzi, siku moja kabla ya kuapishwa akafariki dunia.

 

Alhamisi, 1 Machi 2018

ROMA MKATOLIKI AFUNGIWA MIEZI 6 KIMUZIKI

Msanii wa muziki wa Hip Hop bongo Roma Mkatoliki amefungiwa kufanya shughuli za muziki kwa muda wa miezi sita kwa kile kilichodaiwa msanii huyo kudharua wito wa BASATA na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
By zakaboyblog Mtz midia facebook
Akiongea na waandishi wa habari Naibu Waziri   
 wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Juliana Shonza amesema kuwa amechukua maamuzi hayo kutokana na kumwita msanii huyo ili aweze kufika kwenye mkutano huo lakini hakuweza kufika wala hakutoa taarifa yoyote ile. 
"Roma Mkatoliki alipigiwa simu na BASATA hapokei na anatumiwa message anasoma lakini hajibu kitu, kwa hiyo kimsingi hilo ni kosa kwa sababu tumemuita si kama tumekurupuka bali Roma Mkatoliki aliutoa wimbo wake muda kidogo unaitwa Kibamia kimsingi ule wimbo ameimba matusi matupu na ni wimbo ambao kiasi fulani unadhalilisha kwa sababu mtu unapozungumzia kibamia huitaji kujiuliza kibamia ni nini kila mtu anajua maana ya kibamia, mimi siamini hata mtu ambaye yupo hivyo anakuwa amependa" 
Juliana aliendelea kutoa ufafanuzi kuhusu suala la Roma Mkatoliki 
"Nakumbuka mwaka jana nilikuagiza Mkurugenzi wa BASATA kwamba umwite Roma Mkatoliki ukae naye chini, kwenye onyo lake la kwanza mwambie afanyie marekebisho huo wimbo na uzuri BASATA walimwita wakaa naye chini wakamwambia kasoro za wimbo wake na kutakiwa kufanya marekebisho ya wimbo huo ikiwepo jina lenyewe la Kibamia, pamoja na baadhi ya matusi ambayo yapo kwenye huo wimbo. Roma Mkatoliki alikubali na kusema ataenda kufanyia marekebisho hizo sehemu cha kusikitisha mpaka saizi napoongea hakuna ambacho kimefanyika na mbaya zaidi wimbo huo unaendelea kupigwa kwenye vyombo vya habari" 
"Roma Mkatoliki amedharau maagizo ambayo alipewa na BASATA na kwa sababu tumemwita leo na hajafika bila taarifa yoyote hivyo amedharau wito, mimi kama Naibu Waziri wa Habari pamoja na BASATA tumekubaliana kwamba huyu ndugu Roma Mkatoliki tunampa adhabu kwa mujibu wa Katiba na kanuni, hivyo tunamfungia kwa muda wa miezi sita ndani ya muda huo wa miezi sita hakuna kufanya kazi yoyote ya sanaa, hakuna kutoa wimbo wowote, hakuna kufanya show sehemu yoyote, huo wimbo moja kwa moja tunaufungia" alisisitiza Shonza 

Jumanne, 27 Februari 2018

WASAFI TV WASAFI FM SI KWAAJILI YA MASHINDANO KWA VYOMBO VYA HABARI VINGINE

Msanii Diamond Platnumz amesema Wasafi FM na TV si kwa ajili ya mashindano na vyombo vingine vya habari.

Akizungumza visiwani Zanzibar Diamond amesema vyombo hivyo ni kwa ajili ya kuondoa matabaka miongoni mwa wasanii na kukuuza muziki.
“Ninaomba watu waelewe kabisa hakipo katika kushindana na kitu chochote au kushinda na chombo chochote,” amesema Diamond.
Diamond na timu yake ya Wasafi kwa sasa wapo visiwani Zanzibar kwa ajili ya kusaka vipaji vya utangazaji ambavyo vitapewa nafasi katika vyombo hivyo vya habari.

Jumatano, 14 Februari 2018

JUMATANO YA MAJIVU KUAZIMISHWA

               By zakaboyblog
TUMSIFU YESU KRISTO?*

*Leo nakukaribisha ujifunze kuhusu kipindii tunachoelekea*

*Makinika*

Seminarian Gabriel 

*" Ijuwe jumatano ya majivu kiundani "*

Jumatano ya Majivu, katika kalenda ya mwaka wa Kanisa la Magharibi, ni siku ya kwanza ya kwaresima, walau kwa madhehebu mengi.

Jina linatokana na desturi ya kumpaka mtu majivu kichwani pamoja na kumtamkia maneno ya kumhimiza afanye toba inavyotakiwa na kipindi hicho cha liturujia kinachoandaa Pasaka.

Kwa kawaida siku hiyo unaanza mfungo unaofuata kielelezo cha Yesu kufunga chakula siku arubaini jangwani baada ya kubatizwa na Yohane Mbatizaji na kabla ya kuanza utume wake mwenyewe.

Wakati umetimia na ufalme wa Mungu umekaribia, tubuni na kuiamini Injili, (Mk 1:15), haya ndiyo maneno ya kwanza ya Yesu ambayo kadri ya Mwinjili Marko yanafungua kazi ya hadhara ya Yesu, kwa maana hiyo kazi ya Yesu inaanza kwa kuwaandaa watu katika toba ili hatimaye, wapate kuukaribia au kuingia katika ufalme wa Mungu. Na wakati ndiyo sasa. Wakati ni sasa , Yesu anatuhubiria na Kwaresima imewadia, na ndiyo maana siku ya Jumatano ya majivu, kwa kuitikia mwito wa maneno ya Yesu kanisa linatualika kuingia katika kipindi cha Kwaresma, ambacho ni kipindi cha kujikusanya, kujitayarisha, kijitengeneza na kujikarabati hasa kwa toba, kufunga, kusali na kujitoa sadaka zaidi mambo yanayorutubishwa kwa tafakari ya kina ya Neno la Mungu.

*NINi MAANA YA JUMATANO YA MAJIVU ?*


Jumatano ya majivu ni mwanzo wa kipindi cha kwaresima katika kanisa, Ni mwanzo wa siku arobaini za kutafakari kwa undani fumbo kuu la upendo wa Mungu linalofunuliwa kwa kujitoa kwake na kufa msalabani, kifo cha aibu cha Msalaba ili kuichukua aibu yetu au dhambi zetu.

*KWARESMA NI NINI ?*

Kwaresma ni kipindi cha siku 40 cha kujiandaa kuadhimisha Sherehe kuu ya PASAKA yaani kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Tunajiandaa kwa Kufunga Kusali, Kutubu, na Matendo mema.
Mama kanisa anatupatia kipindi hiki ili tuweze kutafakari njia na mienendo yetu na kubadilika kama haimpendezi Mungu

Tunapofunga tunatakiwa kuzuia vilema vyetu na kuviacha kabisa, tunaomba kujaliwa moyo wa toba, tunainua mioyo yetu na tunaomba Mungu atujalie nguvu na tuzo. Haitoshi tu kukiri makosa yetu bali tunahimizwa kuungama na kutubu hayo makosa na kuwa tayari kuanza upya. Kipindi cha Kwaresima huanza tangu Jumatano ya majivu. Mwanzoni mwa kazi yake ya kuhubiri Habari njema Yesu anaanza kwa kusema tubuni na kuiamini Injili – Mk 1,15. Maneno haya haya tunayasikia/tumeyasikia kila tunapopakwa majivu. Mwaliko huu wa Yesu unatuingiza katika kipindi cha toba – tubuni na kuiamini Injili. Huu ni mwaliko wa uzima. Ni mwaliko ili tuongoke, tuanze maisha mapya, maisha ya sala, kufunga na kutoa sadaka.

*KWA NINI IKAITWA JUMATANO YA MAJIVU ?*


Jina linatokana na desturi ya kumpaka mtu majivu kichwani pamoja na kumtamkia maneno ya kumhimiza afanye toba inavyotakiwa na kipindi hicho cha liturujia kinachoandaa Pasaka.

Kwa kawaida siku ya Jumatano ya majivu unaanza mfungo unaofuata kielelezo cha Yesu kufunga chakula siku arubaini jangwani baada ya kubatizwa na Yohane Mbatizaji na kabla ya kuanza utume wake mwenyewe.

*MAJIVU TUNAYOPAKA YANA MAANISHA NINI ?*


Majivu ni ishara ya majuto, nayo hufanywa visakramenti kwa kubarikiwa na kanisa. Tunapopakwa majivu katika paji la uso hutusaidia kutafakari na kutukumbusha kuwa wanadamu sisi tu mavumbi na mavumbini tutarudi. Hutukumbusha zaidi kuwa maisha ya hapa duniani tunapita na safari yetu itakamilika pale tutakapoungana na Bwana na mwokozi wetu katika ufalme wako.
Angalia; Isaya 61:3, Ester 4:1-3, Yeremia 6:26, Ezekieli 27:30, Mathayo 11:21 na Luka 10:13

*KWA NINI MAJIVU YANAPAKWA KWENYE PAJI LA USO NA SI PENGINE.*

Ishara yoyote iwekwayo katika paji la uso huonesha umiliki (soma Ufunuo 7:3, Ufunuo 9:4, Ufunuo 14:1, Ezekieli 9:4-6, ). Tunapochorwa ishara ya msalaba katika paji la uso ni ishara kwamba sisi tupo chini yake yeye aliyekufa msalabani kwa ajili yetu.
Hali kadhalika hutukumbusha ishara ya msalaba tuliyochorwa na mafuta matakatifu siku ya ubatizo wetu, hutukumbusha ahadi tuliyoiweka siku hiyo ya ubatizo na kutuita tuishi maisha ya utakatifu

*PADRE UTAMKA MANENO GANI WAKATI ANAPAKA MAJIVU ?.*

Tunapopakwa majivu Padre husema; Mwanadamu kumbuka u mavumbi na mavumbini utarudi AU Tubuni na kuiamini Injili.
Maneno anayosema padre yana maana gani?

Maneno haya kwa upande mmoja hutukumbusha tunapoelekea, tusisikitike kwamba siku moja tutarudi mavumbini bali tuwe na furaha kwani wakati miili yetu unarudi mavumbini roho zetu zitakwenda kuungana na Mungu Baba mbinguni.
Hivyo maandalizi tunayoalikwa kuyafanaya si maandalizi ya kuelekea mavumbini bali maandalizi ya kuelekeza roho zetu mbinguni. Ndio maana pia twaambiwa tubuni na kuiamini Injili.

*MAJIVU TUNAYOPAKWA YANATOKA WAPI ?*

Majivu tunayopakwa hutoka katika matawi yaliyotumika katika jumapili ya matawi ya mwaka jana. Majivu haya hubarikiwa na kuwa visakramenti. Hivyo majivu yanapoashiria toba na majuto pia hutukumbusha wema wa Mungu na utayari wake wa kutusamehe.

*KWA NINI TUNATUMIA MATAWI YA JUMAPILI YA MATAWI ?*

Matawi haya yalimkaribisha Yesu Yerusalemu akiwa tayari kufa kwa ajili ya dhambi zetu, yalimpokea mfalme kwa furaha na shangwe kuu. Matawi haya yanapochomwa na sisi kupakwa majivu yetu yanatukumbusha kuwa ni kwa ajili ya dhambi zetu Mungu alimtoa mwanae wa pekee kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu sisi wanaadamu. Hivyo hututafakarisha kuacha dhambi.

*KANISA LIMEKATAZA NINI SIKU YA MAJIVU ?*

Tumekatazwa kula chakula siku ya Jumatano ya Majivu na kula nyama siku ya Ijumaa Kuu katika Amri ya Pili ya Kanisa.
Nani analazima kufunga siku ya Jumatano ya majivu na Kwaresma?

Kila Mkristo aliyetimiza miaka 14 na zaidi anapaswa kufunga kula nyama (Ijumaa kuu) na mwenye miaka zaidi ya 21 kufunga chakula Jumatano ya Majivu

*TUNAPOSEMA KUJINYIMA WAKATI WA KWARESMA TUNAMAANISHA NINI ?*

Kujinyima ni kujikatalia kitu ukipendacho mfano nyama, pombe, sigara, muziki, safari, maongezi n.k.

*HITIMISHO*

Wakati wa Kwaresma Waamini wanapaswa kujitakasa zaidi kwa kusali, kufunga, toba na matendo mema

Kipindi cha Kwaresima ni fursa makini ya kumkimbilia Mwenyezi Mungu, kwani kwa njia ya dhambi wamejikuta wakiwa mbali na Uso wa huruma ya Mungu, kiasi hata cha kupoteza imani na matumaini kwa Mwenyezi Mungu. Hii ni changamoto ya kumpenda Mungu na jirani badala ya kukumbatia malimwengu yanayoendelea kuwatumbukiza katika utupu wa maisha ya kiroho. Kwaresima ni kipindi cha waamini kukimbilia na kuambata huruma ya Mungu inayoganga na kuponya dhambi. 

Ni wakati wa sala, upendo na kufunga.
By zakaboyblog
Yout