JINSI YA KUMSHUGULIKIA MTU AKUSEMAYE VIBAYA AU MWENYE ROHO MBAYA
Mtu mwenye Roho mbaya ana majina mengi na ana nazo sifa nyingi zinazo mtambulisha na wanapatikana katika kila nyanja ya maisha. Toka kwa Mtoto mdogo hadi mkongwe ,Msomi na hata asiye msomi muumini wa Dini na kwa wapagani pia.Wao sifa zao kubwa ni kuzungumza ya watu na kulaumu wengine kuwa wana makosa. Watu wa jinsi hupenda kuua ujasiri wako kwa kukulaumu hata kwa matendo ambayo hukufanya au umefanya lakini ilikuwa sio kwa nia mbaya.Hupenda kubadili habari njema yako kuwa mbaya hubadilisha mtazamo wako .Mara nyingi husababisha wewe uwe na msongo wa Mawazo na Afya Mbaya.watu wa jinsi hii huyafanya maisha yako kuwa ya Mashaka na upweke.Masengenyo yao na ubaya wao huusambaza ili maisha yako yaharibikiwe na uonekane duni katika jamii na Ndugu zako.
Kuwa shughulikia watu wa jinsi hii huwa ni ngumu na hasa wale wenye tabia ya kulaumu na kusambaza lawama kwa Jamii .Ndugu na rafiki zako.Mara nyingi jambo baya likitokea katika jamii mara nyingi kulielekeza kwa wengine iliwao wasionekane wabaya kwa kukusukumia lawama.Kuwashughulikia watu wa Jinsi hii mara nyingi hukuacha uwe na Msongo wa mawazo na kuwa na Afya mbaya .Ushauri mzuri ni kuwapuuza na kuwatoa katika mzunguko wa maisha yako.Sio rahisi kuwatambua watu wenye tabia mbaya kirahisi kwakuwa wanakuja katika kila aina ya Maisha ya Binadamu.Nita kwenda kujadili sifa chache ambazo zita mtambulisha mtu mwenye Roho mbaya na Baadae nitatoa njia ya jinsi ya Kuepukana nao .
SIFA ZA DALILI ZA MTU MBAYA
1Mtu mbaya huwa hakubali kuwa amefanya kosa hata kama amekosea atatafuta njia ya kuipeleka lawama kwa mwingine au atatengeneza kila njia kuhakikisha anamkoseha mwingine kwa kumshauri vibaya au kumshawishi atende jambo baya ililile kosa alilofanya yeye lihamie kwa mwingine aionekane yeye kuwa amehusika na kosa hilo.Na hawa ombi msamaha kokote kwakuwa wao wanajiona kuwa hawana hatia.
Na hata wakiomba msamaha huwa ni wa kinafiki bado wakikurudishia lawama kwako kwamba kama usingelikuwa wewe wasingalikosea hivyo ni kwa makosa yako ndiyo maana wamekosea.Mara nyingi watu kama hawa hupata sifa yakufanya vizuri kama tatizo likiisha vizuri na wewe kuonekana kama hufai mbele za wengine yeye akiwa ana faa zaidi yako.
2.Mtu mbaya kukataa hata kama amefanya kitu kibaya hakubaki kuwa amekifanya yeye hata kama unaushahidi wa kutosha atakataa na aatsema kuwa wewe ni mwongo atabisha kwa kuwa watu kama hao huwa hawayakubali makosa yao.Hata kama wanajua kuwa wamekosea mtu mbaya atendelea kubisha tu iliaonekane kuwa hana hatia hata kama anayo hatia ya kosa alilolifanya na ushahidi upo lakini ataendelea kubisha na kutafuta namna ambayo aonekane ni mwema na wewe ni mbaya.
3Mtu muovu hushangilia na kuyatangaza mambo yako kwa wengine haraka sana anapokugundua umefanya makosa .sababu kubwa ili yeye aonekane kuwa ni mwema kwa jamii na ndugu wewe ni mbaya sana .Watu wabaya hujitahidi sana kukupiga majungu iliusifanikiwe na hasa wakiona umepata fursa ambayo wao pia wanaweza kuipata hujitahidi sana kutapakaza uvumi wa uongo haraka sana iliiwezekusikika na kwa uovu wao wata kusema vibaya ili ukate taama usifanikishe katika fursa iliyojitokeza ili wao waichukue fursa hiyo.
4Bahati mbaya sana watu wabaya huwa hawajitambui kuwa ni wa baya kiasi gani.Na huwa hawa sikii maumivu au hisia ya uchungu wanayokufanyia.Na hata wakijua kuwa umetambua uovu wao watakuambia nilikuwa na kutania tu maana wao wema kwao kumetiwa ganzi na wanafurahia kukuumiza kwa maneno au kwa maandishi yao.Hufurahi kukukebehi wakiwa wanajua kuwa wana kuumiza wao haiingii Akilini mwao kuwa wanatenda lakukuumiza kwakuwa wanafurahia kuumia kwako..
5Watu wabaya Wanaamini kuwa mahitaji yao ni ya muhimu kuliko yako.Matakwa yao na mahitaji yao ni ya muhimu kuliko yako.Hupenda sana kuutumia mgongo wako kuficha uovu wao iliwao wapate na wewe ubebe lawama zao.
6.Tabia nyingine mbaya ya watu hao ukijihami kutokana na tamia mbaya yao watakuzulia jambo na kulitangaza vibaya iliuonekane wewe ni mbay
By zakaboyblog.blogspot.com