Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepata ushindi katika uchaguzi mdogo wa marudio ya ubunge katika majimbo ya Songea Mjini, Singida Kaskazini na Longido.
Akitangaza matokeo hayo Singida Kaskazini msimamizi wa uchaguzi, Rashid Madoa amemtangaza Justine Monko kuwa mshindi baada ya kupata kura 20,857 sawa na asilimia 93.5.
Alisema wagombea wengine na kura walizopata katika mabano ni Dalphine Maloa wa CUF, (974), Aloyce Nduguta w ADA-Tadea (265), Omari Sombi wa AFP (116), Mchungaji Yohana Labisu wa CCK (86).
Alisema kura zilizopigwa ni 22,298, waliojiandikisha kupiga kura wakiwa 91,518 ambapo watu 69,220 sawa na asilimia 70 waliojiandikisha hawakujitokeza kupiga kura.
Katika jimbo la Songea mjini, msimamizi wa uchaguzi Tina Semkambo alimtangaza Dk Damas Ndumbaro kuwa mshindi kwa kupata kura 45,762 sawa na asilimia 97.
Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Longido, Juma Mhina alimtangaza Dk Steven Kiruswa kuwa mshindi akipata kura 41,258 sawa na asilimia 91.5.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni