By zakaboyblog.blogspot.com
IFAHAMU CHAPA YA MNYAMA NA SANAMU YAKE;Somo hili ni mwendelezo wa somo linalosema chimbuko la Taifa la Marekani
YAFUATAYO NI MAMBO TUNAYOJIFUNZA HAPA
I. MNYAMA ANAWAKILISHA - Ufalme au Taifa
UFUNUO 7:17 Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea Duniani.
II. MNYAMA ATAKAVYONENA KAMA JOKA
Mnyama mwenye pembe mbili - Huwakilisha Taifa la Marekani
UFUNUO 13:11-14 Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka. Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona. Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu.Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi. MAELEZO YA ZIADA
KATIKA KITABU CHA TUMAINI KUU SURA 25,UK 275
Pembe kama za mwanakondoo na sauti ya joka vinaonesha ukinzani utabiri kwamba ATANENA “KAMA JOKA na kutumia nguvu zote za yule mnyama wa kwanza unaonesha roho ya kutokuvumiliana na mateso ya yule joka na yule mnyama aliye mfano wa chui. na ule usemi kwamba yule mnyama mwenye pembe mbili AIFANYA DUNIA NA WOTE WAKAAO NDANI YAKE WAMSUJUDIE MNYAMA WA KWANZA .unaonesha kwamba mamlaka ya Taifa hili italazimisha utii kwa mamlaka ya PAPA
Kitendo kama hicho kitakuwa kinakinzana na mfumo wake wa taasisi huru .Tamko la uhuru na katiba inasema Bunge halitatunga sheria inayopendelea taasisi ya kidini au kuzuia uhuru wa kidini na kwamba hakuna sharti la kidini litakalozingatiwa kama sifa ya kuchaguliwa kushika ofisi yoyote ya serikali iliyo Nchini Marekani katika kielelezo hiki KUMEONENYESHWA UVUNJAJI WA MAKUNDI WA MIHIMILI HII YA UHURU.Mnyama mwenye pembe kama za mwana kondoo ambaye kwa maneno ni msafi,mpole na siye na madhara –ATANENA KAMA JOKA
III. NJISI SANAMU YA MNYAMA ITAKAVYOUNDWA
ILI MAREKANI IUNDE SANAMU YA MNYAMA ni lazima mamlaka za kidini zidhibiti utawala wa kiraia kiasi kwamba serikali itatumiwa pia na kanisa kutimiza makusudi ya kanisa
Tofauti kubwa ya imani katika makanisa ya KIPROTESTANTi inachukuliwa kama ushahidi kwamba hakutakuwa na mwafaka wa lazima.lakini kwa miaka kadhaa kumekuwa na mwelekeo miongoni mwa MAKANISA YA KIPROTESTANTI wa kutaka mwungano.ili kuwa na mwungano wa aina hiyo ,MIJADALA YA MAMBO AMBAYO WOTE WALIKUWA HAWAKUBARIANI ITABIDI IWEKWE KANDO. katika juhudi za kufikia mwafaka kamili , itakuwa imebaki kidogo tu kugeukia matumizi ya nguvu
MAKANISA MAKUBWA YA MAREKANI yakiwa yameungana katika masuala ya mafundisho yanayoshikwa na wote ,yatakapoishawishi serikali kulazimisha imani zao na kuunga mkono taasisi zao,MAREKANI YA KIPROTESTANTI itakuwa IMEUNDA SANAMU YA UTAWALA WA KANISA LA ROMA na taabu ya adhabu za kiserikali kwa wanaopinga itafuata bila shaka
IV. KUTIA PUMZI KATIKA ILE SANAMU YA MNYAMA
UFUNUO 13 :15
Akapewa kutia pumzi ka tika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. MAELEZO YA ZIADA
KITABU CHA TUMAINI KUU SURA YA 25,UK 279
Waandishi wa kikatoliki huelezea badiliko hilo kama ishara ya mamalaka ya kanisa Katoliki wakisema kitendo cha KUIBADILI SABATO kwenda JUMAPILI ,jambo ambalo WAPROTESTANTI wanaliafiki......kwani kwa kushika jumapili ,wanakiri uwezo wa kanisa kuweka sikukuu na kuamuru zishikwe CHINI YA DHAMBI
Sasa badiliko la sabato nini? kama siyo ishara au alama ya mamalaka ya kanisa la Rumi –Alama ya manyama ? kanisa la Roma halijakanusha madai yake ya ukuu .ulimwengu pamoja na makanisa ya KIPROTESTANTI wanapoafiki sabato iliyowekwa na kanisa hilo huku wakiikataa sabato ya biblia kimsingi wanakubaliana na madai hayo kwa kufanya hivyo wanaipuuza kanuni ambayo inawatofautisha na kanisa la Roma isemayo biblia ,biblia pekee ndiyo dini ya waprotestanti kadiri harakati za kulazimisha
By zakaboyblog.blogspot.com