by Zakaboy blog
1.Chuki ikikujaa moyoni itakufanya uone kila kitu kibaya na utakua negative zaidi, hata kama kitu kina mazuri yake utapinga hata kwa makusudi ilimradi useme mabaya yake tu
2. Utapata presha na kihoro kwajili hata ya mambo ya kawaida na yasiyokuhusu.
3.Utajikuta unafanya vitu vibaya ambavyo utajutia sana, sababu utafanya ili ujifurahishe wewe, jiulize ukimuumiza mtu asiye na hatia makusudi were utapata nini ukimuona bado anaendelea kuishi kwa amani? si utatamani na uhai wake?!
4.Chuki hupandikiza na hupandikizwa hakuna mtu anazaliwa na chuki, jiepushe na mitazamo has I na kufuata mkumbo.
5.Hakuna jambo hutatuliwa kwa chuki ila upendo, maranyingi watu wenye chuki au kutaka kutatua tatizo kwa chuki maranyingi hukosa maarifa hivyo kuishia kufeli sababu chuki hupumbazwa na hasira, ukipanda ulingoni na hasira utapigwa tu.
6.Chuki binafsi huleta umasikini na watu wachuki binafsi hawanaga maendeleo. Jirani yako alokuzidi akinunua gari usichukie bali hamasika, chukia hali yako ya umaskini ili ufanye kazi kwa bidii utoke kimaisha na ukijichukia mwenyewe hapo umefeli mazima.
7.Chuki huleta wivu, uchawi, masimango, vinyongo, ubaguzi, utumwa wa fikra, chuki ni mateso ambayo huanza na we we mwenyewe
8.Chuki itakuzeesha, itakukondesha, wewe ni shabiki na unamchukia staa ambae hujawahi hata kumuona na hakujui, yeye na matatizo yake akilia analia na Mungu wake wewe, wewe una matatizo yako, unaongeza ya maishan yake sumu.
9.Chuki ni sumu mwilini unaouchosha mwili kwa (stress), chuki nzuri ni ya kimaendeleo chuki nzuri ni ya kuwa na kiu ya kuinua hali ya maisha yako.