Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Habari za kitaifa. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Habari za kitaifa. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 21 Februari 2020

LUGORA NA ANDENGENYE WAKUTWA NA MAKOSA

  LUGOLA NA ANDENGENYE WAKUTWA NA MAKOSA

Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU imesema uchunguzi wa sakata la manunuzi ya vifaa vya zimamoto na uokoaji yasiyozingatia sheria na taratibu za nchi ambao ulisimamiwa na aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani KANGI LUGOLA na aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto THOBIASY ANDENGENYE umekamilika kwa asilimia 99.9

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brig. Jenerali John Mbungo, ameviambia vyombo vya habari kuwa uchunguzi umebaini makosa mengi katika mkataba wa manunuzi hayo ambayo kwa pamoja yanatengeneza kosa la uhujumu uchumi.

Baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo TAKUKURU wanapeleka taarifa ya uchunguzi huo kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali tayari kwa hatua za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote 17 wa sakata hilo.

NINI MAONI YAKO Usisahau KU-LIKE na KU-SHARE ukurasa wetu ili uwe karibu na habari zote pindi zinapochipuka.

Jumatano, 7 Machi 2018

MUNGU HATANIWI SOMA HISTORI HIZI UONE KAMA MUNGU HATANIWI


1. Mtengenazaji meli ya titanic.
Baada ya kutengeneza meli ya TITANIC, mwandishi wa habari alimuuliza ni kiasi gani ilikuwa salama, nae akajibu " Ni salama sana na haiwezi kuzama na hata mungu hawezi kuizamisha".
Nafikiri unajua kilichotokea kuhusu TITANIC

2.AZUZA (mwanamuziki brazil)
Alipokuwa kwenye show yake ndani ya jiji la Rio dejeneiro , alichukua sigara akaanza kuvuta, akachukua nyingine kisha akairusha juu na kusema " Mungu na hiyo yako , chukua na wewe uvute. Alifariki akiwa na miaka 32 kwa ugonjwa wa kansa ya mapafu, ambayo iliharibu sana mapafu yake kuliko mgonjwa yeyote.

3.Christina hewt (mwandishi)
Huyu alikaririwa akisema " Nimesoma vitabu vyote duniani, ila hakuna kitabu kibaya kama biblia, siku chache baada ya kusema maneno hay, mwili wake ulikutwa umeunguzwa moto ambao haijajulikana hadi Leo umesababishwa na nini.

4. John Lennon (muimbaji)
Wakati alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari la gazeti la america alinukuliwa akisema " ukristo utakufa na kutoweka duniani, siwezi kuwa na wasiwas na hilo kwa kuwa Nina uhakika nalo. Huyu naye baada ya mda alikutwa amekufa nyumbani kwake

5. Tancredo neves (rais wa brazil)
Alisema kwamba endapo angeshinda kura laki tano katika uchaguzi mkuu Brazil na kuwa rais , hata mungu asingeweza kumtoa katika urais huo. Akafanikiwa akapata kura zaidi ya laki tano akashinda uchaguzi, siku moja kabla ya kuapishwa akafariki dunia.

 

Ijumaa, 12 Januari 2018

SERIKALI KUCHUNGUZA KUHUSU MELI YA TANZANIA KUKAMATWA UGIRIKI

SERIKALI imesema inachunguza taarifa za meli iliyokamatwa nchini Ugiriki ikiwa na bendera ya Tanzania ikipeleka vilipuzi Libya.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Susan Kolimba, akizungumza na Nipashe jana kuhusu tukio hilo, alisema wanafuatilia kwa kina ili kupata ukweli wake.
“Kwa sasa ni kwamba jambo hilo tunalifuatilia ili kujua habari hizo kama zina ukweli na tutakapopata taarifa tutawajulisha, bado tunafuatilia,” alisema Kolimba.
Jana, Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) ilieleza kuwa maofisa wa Ugiriki wanaofanya doria baharini  wameizuia meli hiyo iliyokuwa inapeperusha bendera ya Tanzania ikiwa imebeba vilipuzi.
Taarifa hiyo ya BBC ilieleza kuwa meli hiyo inadaiwa kusafirisha vilipuzi hivyo kutoka Uturuki kwenda Libya, kinyume cha sheria iliyowekwa ya kutosafirisha silaha kwenda Libya.
Iliongeza kuwa maofisa hao wameeleza kwamba meli hiyo ilikuwa imebeba kreti 29 zilizojaa vilipuzi pamoja na kemikali zinazotumiwa kuunda vilipuzi.
"Maofisa wa kushika doria baharini wamezima bomu lililokuwa linasafiri," ofisa mkuu wa walinzi hao wa Ugiriki, Yiannis Sotiriou alikaririwa na BBC jana.
Taarifa ya BBC ilieleza kuwa Wizara ya Safari za Baharini ilisema meli hiyo ilisimamishwa ikiwa katika kisiwa cha Crete kusini mwa Ugiriki baada ya maofisa kupatiwa taarifa na ilisindikizwa hadi katika bandari ya kisi wa hicho na kufanyiwa ukaguzi.
Sotiriou alikaririwa katika taarifa hiyo akieleza kuwa meli hiyo ambayo ilinaswa Jumamosi ilikuwa pia na kasoro nyingi na haikufaa kuwa baharini.
"Ingesababisha madhara makubwa sana kwa watu na mazingira pia," alikaririwa katika ripoti hiyo ya BBC.
Ilielezwa zaidi katika ripoti hiyo kuwa nahodha wa meli hiyo ambaye alifahamika kwa jina moja la Andromeda, alidai meli hiyo ilikuwa inasafiri kuelekea Djibouti lakini baadaye ikabainika kwamba ilikuwa inasafiri kuelekea mji wa bandarini wa Misrata nchini Libya.
Kwa mujibu wa ripoti ya BBC, mabaharia wanane ambao ni raia wa India, Ukraine na Albania waliokuwa kwenye meli hiyo, walitarajiwa kufikishwa mbele ya mwendesha mashtaka jana.


200