Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lafahamisha kukutana kwa dharura ili kujadili uamuzi uliochukuliwa na rais wa Marekani kuhusu jiji la Jerusalamu.
Trump alitangaza rasmi Jumatano kuwa serikali yake inatambua jiji la Jerusalem kama mji mkuu wa Israel licha ya kutahadharishwa na viongozi tofauti ulimwenguni akiwemo Papa Francis kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni.
Mkutano huo umetolewa wito na Uruguay punde tu baada ya muda mchache Trump kutangaza kulitambua jiji la Jerusalemu kama mji mkuu wa Israel.
Uruguay, Ufaransa, Bolivia, Misri, Senegal, Uswidi, Uingereza na Italia ndio wanachama wa Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa watakaoshiriki katika mkutano huo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni