Alhamisi, 7 Desemba 2017

Waislamu na wakristo waungana kupinga uamuzi wa Trump kuhusu Jerusalem

Waislamu na wakristo washirikiana kupinga uamuzi wa Trump kutangaza kutambua mji wa Jerusalem kama mji mku wa Israel kwa kuzima mataa mskiti wa al Aqsa kwa waislmu huku wakristo wakizima mataa yaliokuwa yamewashwa katika viashirio vya uzawa wa Yesu Noeli.

Baada ya kutangazwa mji wa Jeusalem kama mji mkuu wa Israel  mataa yote yalizimwa Ukingo wa Magharibi.

Viashirio vyote vya uzawa wa Yesu katika kanisa la Betlehemu  vilizimwa ishara ya kupinga uamuzi huo wa Trump.

Azimio nambari 478 lka Umoja wa Mataifa la mwaka 1980 linatupilia mbali kutangazwa kwa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.

Mataifa yote yanayoheshimu azimio hilo yalifungua balozi zao mjini Tel Aviv.

Hakuna maoni: