Kilo 55 za mapembe ya tembo na mikia 46 yakamatwa mjini Abidjan nchini Ivory Coast
Washukiwa wanne wa ulanguzi wa mapembe ya tembo wamekamatwa katika operesheni ilioendeshwa na jeshi la Polisi wakiwa katika hatakati za kuuza mikia 46 na kilo 55 za mapembe ya tembo mjini Abidjan.
Msako mkali umeendeshwa katika kitongoji cha Trenshville Kusini mwa jiji la Abidjan katika kituo cha mchongaji vinyago.
Mikia 46 ya tembo imekamatwa, kwa mujibu wa taarifa mikia hiyo inatumiwa kwa kutengeneza urembo kwa ajili ya wanamume.
Mkia wa tembo unatumiwa kwa ajili ya ujenzi wa mikanda ya saa au mikandaa pekee ambayo wanamume huvaa kwa ajili ya urembo.
Mkanda mmoja huwa ukiuzwa kwa thamani ya dola 2000.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni