Chama cha wamiliki wa Mabasi-TABOA kwa kushirikiana na chama cha wamiliki wa daladala wametangaza mgogoro na mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu SUMATRA na kupanga kuitisha mkutano mkuu wa wamiliki wa vyombo vya usafiri jumapili ijayo ilikutisha mgomo wa usafiri nchni nzima.
Wakizungumza baada ya kutoka katika ofisi za SUMATRA makao makuu, mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa mabasi- TABOA- Bwana Enea Mrutu amesema wamefikia hatua hiyo baada ya SUMATRA kushindwa kutekeleza maoni yao katika kanuni zilizopitisha ikiwemo kutengenisha makosa ya dereva na mmiliki pamoja na kupunguza faini ya shilingi laki 2 kwa ni kubwa mno.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa daladala Bw. Kismati Jafari amesema kanuni hizo zinalenga kutoa adhabu zinazoweza kurudisha nyuma sekta ya usafirishaji kutokana na kutoa adhabu kali ikiwemo kifungo kwa madereva au mmiliki anayeweza kuzuia afisa wa sumatra kufanya kazi yake.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni