Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam shekhe mkuu wa dhehebu la shia ithna sheria Ahmed Jalala amesema tukio hilo la arubaini ya Imamu HUSSEIN ambaye ni mjuu wa Mtume ni tukio la kawaida kwa waumini wa kiislam na wasio kuwa wa kiislam.
Jalala amebainisha mafunzo mbalimbali yatokanayo na tukio hilo ni pamoja na kuuenzi utukufu na heshma ya mwanadamu Duniani pamoja na kujenga umoja upendo amani na mshikamano Nchini.
Aidha amewataka waumini wa dini ya kiislam nma wasiokuwa waislam kuhakikisha mafunzo yanayotolewa kwa vijana kutokuwa na sifa ya ugaidi na badala yake wajikite katika kusimamia amani nchini.
Katika tukio la Arbaini ya Imamu HUSSEIN mwaka huu kauli mbiu yake ni Tusimame Kutetea haki za binaadam na kupinga ugaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni