Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani SACP Fortunatus Musilimu amesema hakutakuwa na msamaha kwa dereva yoyote atakaevunja na kukiuka sheria za usalama wa barabarani huku akiwataka askari wote popote walipo wafanye kazi kwa kujiamini ili kuhakikisha ajali zinapungua nchini.
Kamanda Musilimu ametoa kauli hiyo leo mkoani Kilimanjaro mara baada ya kukutana na wajumbe wa kamati ya Baraza la Usalama Barabarani kwenye maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama yanayoendelea mkoani humo.
Amesema mtu yeyote atakaekamatwa amekiuka sheria za barabarani asitarajie kuwa ataishia kutozwa faini tu bali watafikishwa mahakamani kwa hatua zingine zaidi za kisheria kuchukuliwa.
Amesisitiza kuwa japo watu husema kwa sasa mabasi hutembea kwa mwendo mdogo na kuchelewa kufika kwa wakati hiyo ndiyo chachu kubwa iliyopunguza ajali za barabarani na kuokoa maisha ya watu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni