Jumamosi, 20 Januari 2018

Bodi za wakurugenzi za majisafi, usafi na mazingira zavunjwa

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe hii leo amevunja Bodi za Wakurugenzi za Majisafi na Usafi wa Mazingira za Jiji la Arusha na Musoma.

Kwenye taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari ambayo imesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiy Prof. Kitila Mkumbo, imesema Waziri Kamwelwe amesema kuwa amefanya hivyo baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa Bodi hizo.

Taarifa hiyo imeendelea kuelezea kuwa tayari mchakato wa kuunda bodi mpya umeanza, na zitatangazwa mara zitakapokamilika.

Isome hapa taarifa yote




Hakuna maoni: