Baada ya mfalme wa Saudi Arabia kutoa ruhusa kwa wanawake kuendesha magari,kampuni moja nchini humo imeamua kuanzisha madereva wa teksi wanawake.
Kwa mujibu wa habari,mfalme Salman alitoa idhini ya wanawake kupewa leseni na ruhusa ya kuendesha magari kuanzia Juni mwaka kesho.
Ripoti zinaonyesha kuwa kampuni hiyo ina mpango wa kuajiri zaidi ya wanawake 100,000 kama madereva wa teksi.
Meneja wa kampuni hiyo amesema kuwa itatengenezwa programu ambapo mteja mwanamke ana uwezo wa kumuita dereva wa kike.
Programu hiyo itaweza kuonekana kwa wanawake peke yao.
Haya ni mapinduzi ya hali ya juu kwa nchi kama Saudi Arabia.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni