Jumamosi, 14 Oktoba 2017

Burkina Faso: Kifo cha Thomas Sankara kulipizwa kisasi

Rais wa Burkina Faso amewaahidi wananchi na dunia nzima kuwa kifo cha Thomas Sankara hakitonyamaziwa kimya.

Hayo rais Roch Marc Kabore ameyazungumza katika ikulu ya rais wakati akiongea na rais wa Senegal Macky Sall.

Rais huyo amesema kuwa amehakikisha anatoa amri kwa kitengo chote cha sheria kuhakikisha kuwa kifo cha kiongozi wao bora Thomas Sankara kinatendewa haki.

Thomas Sankara ambae alikuwa rais wa zamani wa Burkina Faso aliuawa Oktoba 15 1987 wakiwemo walinzi wake wawili na dereva.

Aliiongoza Burkina Faso kuanzia mwaka 1983 mpaka wakati wa kifo chake 1987.

Lengo lake lilikuwa ni kupambana na rushwa na uongozi mbaya wa ukoloni wa kifaransa.

Uchunguzi uliofanywa katika mwili wake mwaka 2015 ulionyesha kuwa alipigwa risasi na baadhi ya viungo vyake kuharibiwa vibaya.

Thomas Sankara ni kati ya viongozi bora wa bara la Afrika katika miaka ya 80.

Hakuna maoni: