Alhamisi, 26 Oktoba 2017

Mvua yaathiri usafiri wa mabasi Kasi

Mvua kubwa iliyonyesha jijini Dar es Salaam imesababisha kampuni ya mabasi yaendayo haraka (Udart) kusitisha ​huduma.

Udart imesema leo Alhamisi Oktoba 26,2017 kuwa imesitisha huduma kutokana na eneo la Jangwani zilipo ofisi zake kujaa maji hivyo mabasi kushindwa kupita.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Udart, Deus Bugaywa amesema, "Tumesitisha huduma za mabasi yote kutokana na eneo la Jangwani kujaa maji." Amesema maji yatakapopungua wataanza tena safari kama kawaida.




Hakuna maoni: