Baada ya Mzamiru Yassin kuanza mazoezi hapo jana, Miraji Athumani ndiye mchezaji pekee ambaye anaendelea kuwa nje ya dimba akiuguza majeraha
Miraji amekuwa nje kwa takribani miezi miwili sasa akiuguza majeraha hayo ya goti
Kabla ya kupata majeraha, Miraji alikuwa kwenye kiwango bora akifunga mabao sita
Pamoja na kukosekana kwake Simba imeendelea kufanya vizuri kutokana na ubora wa kikosi chake
Deo Kanda ni mchezaji mwingine aliyekuwa majeruhi lakini tayari amerejea kikosini