Jumatano, 16 Oktoba 2019

KAMA UNA TABIA. HIZI MAFANIKIO KWAKO YATABAKI KUWA NDOTO

Adui wa kwanza wa mafanikio katika maisha yako ni wewe mwenyeweWewe ndiye unayeamua,ufanikiwe au usifanikiwe. Ninaposema hivi nina maana kwamba ziko tabia ambazo ukiwa nazo unafanikiwa na zipo tabia  mbazo ukiwa nazo utaishia kuona wenzako wanafanikiwa wewe unabaki palepale.Tabia hizi ni adui mkubwa wa mafanikio yako.Kwa hiyo usianze kutafuta mchawi wa mafanikio yako,mchawi wa kwanza niwewe. Wewe ndiye mwenye maamuzi ya mwisho juu ya maisha yako unataka yaweje.

Hizi ni tabia ambazo umekuwa nazo kwa muda mrefu na hutaki kuziachia. Kwa jinsi unavyoendelea kuwa nazo ndivyo ambapo unajikuta maisha yako yanazidi kuwa magumu na wakati huo huo mafanikio kwako yataishia kuwa ndoto ya saa sita mchana, ndoto ya alinacha na mara nyingi utajikuta ukiishi maisha ya wasiwasi huku ukiwa hauna uhuru katika maisha yako. Unapojifunza tabia hizi fanya mabadiliko, chukua hatua sahihi za kubadili maisha yako na utafanikiwa.

Hizi ndizo tabia ambazo ukiwa nazo, mafanikio kwako yataishia kuwa ndoto za mchana:-

1.Kutokuwa na malengo.
Ili mtu afanikiwe lazima awe na malengo.Malengo ndio chanzo cha mafanikio, mafanikio hayaji kwa bahatí mbaya. Watu wote waliofankiwa unaowafahamu na usiowafahamu walikuwa na malengo, wakayaweka katika vitendo na kufanikiwa. Kama wewe ni mwanafunzi weka lengo unataka kuwa nani baadaye, vinginevyo utaishia kusoma na kubaki huna kazi ya kufanya; unakuwa umepoteza muda bure katika maisha yako.

Kama wewe ni mfanyabiashara weka lengo la kuwa mfanyabiashara mkubwa. Zingatia kwamba malengo ndiyo yanakupa dira na muelekeo katika maisha yako. Kupitia malengo unajua unatakiwa uanzie wapi na uishie wapi kulingana na lengo ulilojiwekea kwa wakati huo. Kutokuwa na malengo katika maisha ni sawa sawa na kusafiri bila kujua unaenda wapi. Hii ni hatari sana kwako.

By zakaboyblog 0763230371


2 .Kutokuwa na malengo  maalum yanayoeleweka.
Kuwa na malengo haitoshi, ni lazima uwe na malengo yanayoeleweka na kufikika. Ni kosa Kubwa kuwa na malengo mengi Ambayo hayafikiki na kutaka kuyatekeleza kwa wakati mmoja. Kuwa na malengo mengi  humfanya mtu achanganyikiwe. Mtu mwenye malengo mengi ana hatari ya; Kuchanganyikiwa na kushindwa kuamua aanze na lipi, amalize na lipi,pia ana hatari ya kutekeleza mambo nusunusu na hatimaye kushindwa kuendelea kabisa na mipango hiyo.

Weka malengo machache ambayo una uwezo wa kuyatekeleza kwa muda uliopanga kisha anza kutekeleza mpango mmoja hadi mwingine. Ukishafanikiwa kutekeleza mipango hiyo weka lengo lingine na utazidi kupiga hatua moja hadi nyingine na kuzidi kufanikiwa siku hadi siku.

3. Kukosa uvumilivu.
Mafanikio ni safari ndefu sana katika maisha ya binadamu. Mafanikio ya kweli yanachukua muda mrefu kupatikana, hayachukui muda mfupi kama wengi tunavyotaka. Kutaka mafanikio kwa muda mfupi ni tatizo ambalo limetukumba wengi katika dunia ya leo yenye changamoto nyingi za kiuchumi, kijamii na kisiasa. Watu wengi tunaiogopa safari ndefu ya mafanikio, tunataka mafanikio ya muda mfupi.

WatuWengi wanakata tamaa mapema kwa kwa sababu wanataka mafanikio kwa mnuda mfupi jambo ambalo haliwezekani. Matokeo yake wanaamua kupita njia za mkato ili kufikia malengo wanayojiwekea. Usiogope kuchukua muda mrefu hadi kufanikiwa,hayo ndiyo mafanikio ya kweli. Ikiwa unataka kufikiamafanikio, usiogope kupita jangwani.