Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, ameuzungumzia mwaka 2017 huku akiukaribisha mwaka mpya, kwa kusema kuwa tukio la kupigwa risasi Tundu Lissu lilimgharimu sana.
Kwenye ukurasa wake wa facebook Zitto Kabwe amesema kupigwa risasi kwa Tundu Lissu kulimfanya abadili mtazamo wake na kumfanya kupoteza watu wa karibu.
"Tukio la kupigwa risasi Mbunge Tundu Lissu ni tukio baya sana na lilibadilisha kabisa mtazamo wangu wa mapambano ya kulinda Demokrasia. Ilinigarimu kwa kupoteza watu wa karibu kufuatia kuwa mkali sana kulaani tukio lile. Sijutii kwani niliamini kuwa lengo la waliotaka kumwua Lissu lilikuwa kutunyamazisha na hivyo majibu sahihi yakawa ni kusema zaidi", ameandika Zitto Kabwe.
Pia Zitto Kabwe ameendelea kwa kusema kuwa tukio lingine alilokumbana nalo 2017 ni kitendo cha kuondoka kwa wanachama waandamizi na kuhamia chama kingine, huku akilielezea kuwa limekuwa funzo kubwa kwake.
"Kuondoka wanachama waandamizi ilikuwa pigo. Pigo hili limetupa funzo kubwa Sana na hivyo Tutaendelea kuwepo na imara zaidi mwaka 2018", ameandika Zitto Kabwe.
Sambamba na hilo Zitto Kabwe amewatakia Watanzania heri ya mwaka mpya, huku akisema kuwa ulikuwa ni mwaka wenye changamoto kubwa sana.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni