Jumanne, 16 Januari 2018

YANGA YASAINI MKATABA NA KAMPUNI MPYA YA KUTENGENEZA JEZI YA NCHINI ITALIA



Kampuni ya kutengeneza na kusambaza vifaa vya michezo ya Macron yenye makao yake makuu nchini Italia imeingia mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Yanga wenye thamani ya sh bilioni mbili.

Kampuni hiyo itakuwa na kibali cha kutengeneza na kusambaza jezi za mabingwa hao katika michuano yote ya kitaifa na kimataifa pamoja na vifaa vya mazoezi.

Katibu mkuu wa klabu hiyo, Boniface Mkwasa amewaambia waandishi wa habari kuwa mkataba huo utakomesha kabisa biashara za uuzaji holela wa jezi za mabingwa hao.
"Leo Klabu ya Yanga imeingia mkataba na kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Macron ambao una thamani ya sh bilioni 2 kwa muda wa miaka mitatu," alisema Mkwasa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa masoko wa Macron, Suleiman Karim amesema wamesaini na mabingwa hao kutokana na ushawishi mkubwa walionao katika soka hapa nchini.

"Yanga ni klabu yenye historia kubwa na mashabiki wengi ni moja ya vitu vilivyo tuvutia kuingia nao mkataba huu," alisema Karim.


Hakuna maoni: