Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom, Yanga itawakosa wachezaji watano katika mchezo wao wa kesho wa ligi utakaofanyika katika uwanja wa Uhuru dhidi ya Mwadui FC.
Nyota hao watakosekana kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo majeruhi na kutumikia adhabu.
Msemaji wa mabingwa hao Dismas Ten amewataja wachezaji watakaokosa mchezo huo ni Donald Ngoma, Gofrey Mwashiuya, Thaban Kamusoko na Abdallah Shaibu 'Ninja' ambao ni majeruhi.
Ten amesema mshambuliji Obrey Chirwa nae atakosekana kwenye mchezo huo kutokana na kufungiwa mechi tatu na kamati ya nidhamu ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) iliyotoka jana.
"Maandalizi ya mchezo yamekamilika na wachezaji wana morali ya hali ya juu ili kuhakikisha tunashinda mchezo huu ingawa tunaamini utakuwa mgumu na Mwadui tunaiheshimu," alisema Ten.
Wakati huo huo Ten amesema mshambuliji Amiss Tambwe amerejea na leo asubuhi amefanya mazoezi na wenzake mwalimu atakapoona inafaa atamtumia katika mchezo wa kesho.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni