Timu ya Yanga kesho itapanda Boti kurejea Tanzania bara baada ya kuondolewa kwenye michuano ya Mapinduzi inayoendelea kule visiwani Zanzibar.
Yanga wameondolewa kwenye michuano hiyo leo baada ya kuburuzwa na URA kwenye mchezo wa nusu fainali kwa ushindi wa Penaiti 5-4 baada ya dakika 90 kumalizika bila kufungana.
URA walipata penaiti zote tano lakini yanga walikosa penaiti moja ambayo ilipigwa na Obrey Chirwa.
Wachezaji wa yanga waliopiga penaiti ni
Tshishimbi-alipata
Hassan Kessy-Alipata
Raphael Daud-alipata
Gadiel Michael-Alipata
Chirwa-Alikosa
URA wanamsubiri mshindi wa mechi ya leo saa 2:15 kati ya Azam na Singida united kwa ajili ya mchezo wa Fainali hapo Januari 13,2018
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni