Na. Ahmad Mmow.
BAADHI ya wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara wapo kwenye taharuki kufuatia taarifa tata iliyowataka wanywe uji wa mihogo ili kuepuka kudhurika na mvua ya ajabu inayotajwa ingeanza kunyesha leo katika mikoa hiyo.
Wakizungumza na Muungwana kwa nyakati tofauti kutoka katika wilaya za Masasi, Newala, Nachingwea na Liwale, baadhi ya wananchi wamekiri kutokea taharuki katika maeneo wanayoishi kiasi cha kusababisha baadhi ya watu kushindwa kwenda kwenye shuguli zao kila siku za uzalishaji mali kwa hofu ya kunyeshewa mvua ya ajabu ambayo ingewasababishia kifo au vilema vya kudumu.
Wananchi hao walisema licha ya taharuki iliyosababisha waogope kutembea lakini pia baadhi yao walilazimika kunywa uji wa unga wa mihogo usiku wa manane wakiwa wamesimama katikati ya milango ya nyumba zao ikiwa ni dawa ya kutodhurika na mvua hiyo ambayo hadi sasa haijanyesha.
Mwananchi Happiness Sospeter wa Mtandi wilaya ya Masasi alisema aliamshwa na baadhi ya majirani zake, leo saa tisa usiku nakushauriwa anywe uji wa unga wa mihogo ili asidhurike na mvua hiyo ya ajabu. 5:Alisema alipowauliza walimsikia nani, alisema nani na wapi alijibiwa kwamba wao walisikia kuna mtoto aliyezaliwa huko nchini Msumbiji akiwa na meno 32 ambaye baada ya kumaliza kueleza hayo alikufa.
Happiness alisema watu wengi walilazimika kutwanga makopa (mihogo mikavu) usiku huo ili wapate unga wapike uji. 6:"Wakawa wanachoteana, walikuwa wanakunywa wakiwa wamesimama katikati ya milango ya nyumba zao ikiwa ni sehemu ya masharti ya dawa hiyo, "alisema Happiness.
Happiness ambae alidai hakutaka kunywa hadi athibitishe ukweli wa jambo hilo kwa viongozi wa serikali kupitia vyombo vya habari, alisema kufuatia taharuki hiyo baadhi ya wananchi walijikuta wakishindwa kutoka nje ya nyumba zao kwa hofu ya kunyeshewa mvua hiyo ambayo hadi habari hii inaandikwa ilikuwa haijanyesha.
"Mimi niliamshwa saa kumi namoja alfajiri, nikaambiwa ninywe uji wa mihogo, kuna mtoto amezaliwa hana kichwa amesema kuna mvua itanyesha leo. Yoyote asiekunywa uji uliotengenezwa kwa unga wa mihogo atakufa au kupata ulemavu wa viungo. Kuna watu wamekunywa, lakini mimi sikunywa. Huwa siamini mambo ya aina hiyo,"alisema Hamisi Singa wa kijiji cha Ikungu, wilaya ya Nachingwea.
Hamisi aliongeza kusema kwamba taarifa hizo zilikuwa zinatatanisha. Kwamadai kuwa maelezo yanatofautiana.
"Siyo taarifa sahihi, maana kila anaeulizwa anakuwa hana uhakika naliliko tokea tukio hilo. Tena kunameseji nimepata leo asubuhi zinasema kwamba huko Msumbiji ilikuwa ni siku yao ya wajinga. Kwahiyo meseji zile zilizokuwa na ujumbe wa kuwahofisha watu zilikuwa kwa ajili ya wajinga, "aliongeza kusema Hamisi.
Nae Abdallah Malombe wa kijiji cha Nangano wilaya ya Liwale, alisema alitumiwa ujumbe mfupi wa simu kutoka kwa rafiki na ndugu zake kushauriwa anywe uji wa unga wa mihogo, natayari baadhi ya watu katika kijiji hicho walikuwa wamekunywa. Ingawa yeye alipata jumbe hizo saa sita usiku. Alisema taarifa alizopewa yeye zilisema kuna mtoto amezaliwa Tandahimba mkoa wa Mtwara akiwa na meno, ndiye aliyasema wapike na kunywa uji wa mihogo. Kwamadai kwamba kuna mvua itanyesha na kudondosha wadudu wataowang'ata binadamu na kuwasababishia kifo au ulemavu.
Maelezo ya wananchi hao yanalingana na yaliyoelezwa na Halima Hamisi wa kijiji cha Nambunga, wilaya ya Newala. Bali yeye alisema tukio hilo lilitokea Mueda nchini Msumbiji.
Kufuatia hali hiyo Muungwana ililazimika kuwatafuta wakuu wa wilaya za Masasi, Nachingwea na Liwale ili kupata maoni yao. Hata hivyo juhudi hizo zilifanikisha kumpata wakuu wa wilaya ya Masasi pekee. . Ambapo mkuu wa wilaya ya Liwale na Nachingwea hawakupatikana hewani.
Mkuu huyo wa wilaya ya Masasi, Selemani Mzee alisema taarifa hizo hazikuwa za kweli, kwani mamlaka husika za kiserikali za wilaya za Tandahimba na Newala na Newala ambako inasemekana kuwa ni mahali zilipoanzia zilikanusha kuwepo tukio hilo. Huku akiwaomba wananchi wa wilaya ya Masasi wapuuze taarifa hizo na waendelee kufanya shuguli zao bila hofu.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni