OFISA WA HABARI WA TFF, CLIFFORD NDIMBO.
Yanga kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Boniface Mkwasa, ilisema kuwa TFF inaependelea Simba na kuipanga itumie Uwanja wa Taifa na wao ikiwapangia mechi zao kwenye Uwanja wa Uhuru.
Ofisa wa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo, alisema jana katika taarifa yake kuwa Bodi ya Ligi ndiyo inayosimamia ligi na hupanga mechi kwa kuzingatia viwanja vilivyochaguliwa na klabu.
Ndimbo alisema katika taarifa yake kuwa katika upangaji wa ratiba hizo pamoja na viwanja, Kaimu Mwenyekiti wa Yanga ambaye ni Mwenyekiti wa klabu hiyo ni mmoja wa watendaji wa bodi hivyo hakuna suala la upendeleo kwenye upangaji wa matumizi wa Uwanja wa Taifa.
"TFF hatuamini kama Mkwasa anaweza kuzungumza maneno hayo kwa sababu anaujua utaratibu na anafahamu kuwa Kaimu Mwenyekiti wa Yanga (Clement Sanga) ndiye Mwenyekiti wa Bodi ambaye angempa sababu kwa nini Simba wameruhusiwa kucheza kesho (leo) na Yanga wataruhusiwa kucheza mechi ijayo," ilisema sehemu ya taarifa.
Afisa huyo aliongeza kuwa TFF inasisitiza kufuatwa na kuheshimiwa kwa kanuni na taratibu za mpira wa miguu huku ikiendelea kufanya kazi kwa karibu na Yanga kwenye mambo mbalimbali na kuhakikisha inaisaidia kukabiliana na changamoto zinazotokea kwenye klabu hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni