Alhamisi, 11 Januari 2018
Tanesco yatoa siku nne kwa wadaiwa sugu
Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limetoa siku nne kwa wadaiwa sugu kulipa madeni yao.
Taarifa iliyotolewa na shirika hilo leo Alhamisi imesema kuwa siku hizo zinaanzia Januari 12, 2018 hadi siku ya Jumatatu Januari 15, 2018.
“Baada ya muda huo kuisha shirika litasitisha huduma ya umeme dhidi ya wateja watakaoshindwa kulipa madeni ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua zingine za kisheria,”
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Ofisi za Tanesco zitakuwa wazi siku ya Jumamosi saa 3:00 asubuhi hadi saa 9:00 mchana.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni