Alhamisi, 11 Januari 2018
Bavicha wamjia juu Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM
Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), limetoa tamko la kumshangaa Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shamkuma juu ya kauli yake ya kumshambulia Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu.
Akizungumza na wandishi wa habari Leo, Katibu Mkuu wa Bavicha Mwita Julius alisema wao kama Baraza wameamua kumjibu Shaka ili aache kudanganya umma juu ya kauli yake.
Mapema hivi karibuni Shaka alizungunza na wandishi wa habari ambapo alikosoa kauli yake ya kumpinga Lissu kuwa yeye ndie mwanasiasa wa kwanza kushambuliwa na risasi.
" Tunamshangaa Shaka kwa kutoka mbele za watu kupinga kauli za Lissu, tunamkumbusha kuwa Huyo Karume ambaye aliuawawa kwa kushambuliwa na risasa hakushambuliwa kisiasa na na hata waliomshambuliwa walikamatwa na wengine kuuwawa" alisema Mwita.
Kuhusu kauli ya Shaka kuwa Lissu anatafuta umaarufu, Mwita amemkumbusha Shaka namna ambavyo Lissu alianza harakati zake za kisiasa kabla ya mwaka 1995.
" Niwatake UVCCM wamuangalie Shaka maana anawaharibia sana chama chao, maana Lissu ameanza kutetea wanyonge tangu enzi ya migodi ta Bulynhulu na namna ambavyo alimtetea Marehemu Chacha Wangwe.
" Tunajua Shaka ni kifaranga sisi Bavicha tunamtaka mama wa Kifaranga tunamtaka aliemtuma Shaka aje, Mama yake aje aseme baada ya Lissu kushambuliwa maendeleo yamefikia wapi, Shaka hajielewi na pengine amelazimishwa Kuzungumza mambo ambayo hayaelewi," alisema Mwita.
Mwita alisema kwa mazingira ya sasa ya Nchi wanategemea vijana wapate ajira na kujiajiri na kujitegemea lakini Shaka anakosa takwimu za kuzungumza juu ya ajira za vijana na badala yake anamshambulia mgonjwa ambaye yupo ICU.
Alimtaka Shaka kama kiongozi wa Chama kinachotawala atoke mbele za watu na kuzungumza masuala ya msingi na sio porojo ambazo hazina msaada kwa Watanzania.
" Shaka anapaswa atoke na kuzungumza wapi alipo Ben Saanane( Msaidizi wa Mbowe) alipo Azory (Mwandishi wa Mwananchi) ambao mpaka sasa hawajulikana walipo, " alisema Mwita.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni