Jumapili, 7 Januari 2018

RASMI, HAJI MWINYI ATANGAZA MAAMUZI YAKE KUHUSU KUONDOKA YANGA

Baada ya kuwepo taarifa kuwa beki wa Yanga, Haji Mwinyi yupo katika mipango ya kuondoka klabuni hapo, mchezaji huyo ametoa tamko rasmi kuhusu taarifa hizo.

Mwinyi ambaye siku kadhaa zilizopita alikuwa akisisitiza kuhama klabuni hapo, amebadili mawazo ya kutaka kuachana na timu hiyo na sasa ameahidi kupigania nafasi ya kucheza huku akiwa na ushindani mkali kutoka kwa Gadiel Michael.

Mwinyi  ameweka wazi kuwa hana mpango wake wa kujiunga na AFC Leopards ya Kenya ambayo ilikwua ikimwania na anaelekeza nguvu zake katika kuipigania timu yake ili waweze kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi na michuano mingine inayowakabili.

Akifafanua zaidi, Mwinyi alisema: "Mambo ya kutaka kuhama niliisha achana nayo kwa sasa mawazo yangu ni kuhakikisha naisaidia Yanga kuchukua ubingwa wa Kombe la Mapinduzi pamoja na michuano mingine lakini hilo la kuhamia AFC Leopards tuliache kwanza sipo tayari kulizungumzia," amesema Mwinyi.

Katika mchezo wa kwanza kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi beki huyo alipangwa dhidi ya Mlandege na kuonyesha kiwango cha hali ya juu na kushangiliwa na uwanja mzima.

Tangu kutua kwa beki Gadiel Michael kutoka Azam FC, kumemnyima nafasi ya kucheza Mwinyi jambo lilisababisha akae benchi takribani mechi zote 12 za Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu.

Klabu ya AFC Leopard ya Kenya ilikuwa ikimuhitaji beki huyo kwa ajili ya kuimarisha safu yake ya ulinzi baada ya Mwinyi kufanya vizuri kwenye michuano ya Kombel a Chalenji iliyofanyika mwishoni mwa kwaka uliopita nchini Kenya akiwa na timu yake ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes



Hakuna maoni: