Mwalimu wa shule ya msingi wilayani Liwale atuhumiwa kumpiga na kumuuwa mwanafunzi wa Darasa la pili.
Mwalimu mmoja wa shule ya msingi katika wilaya ya Liwale mkoa wa Lindi anatuhumiwa kumuuwa msichana wa darasa la pili aliyekuwa anasoma katika shule ya msingi Mikunya, halmashauri ya wilaya ya Liwale.
Habari ambazo zilizotufikia zimeeleza kuwa mwalimu huyo leo asubuhi alikwenda shambani watoto wawili, wote wakike.
Ndiko alikompiga na kumsababishia kifo. Imeelezwa kuwa mwalimu huyo anatuhumiwa kumuuwa msichana huyo ambaye alitarajiwa kuingia darasa la tatu mwaka huu amekamatwa.
Huku ikielezwa kwamba mwili wa marehemu umechukuliwa kutoka katika kijiji cha Mikunya nakupelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Liwale. Muungwana inaendelea kufuatilia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni