Jumamosi, 6 Januari 2018

MAKONDA AAHIDI KUIJENGEA NYUMBA FAMILIA YA MWANDISHI WA HABARI ALIYEFARIKI


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda , Leo amehaidi Kuijengea Nyumba ya Vyumba Vinnie (4) Familia ya Mwandishi (mpiga picha) wa Magazeti ya Serikali TSN wanaochapisha Magazeti ya Habari Leo na Daily News Marehemu Athumani Hamis ambae amezikwa Leo katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam.

Ahadi hiyo Imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TSN Dkt. Yonaz kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Mhe Paul Makonda  ambae aliombwa kuisadia familia ya Marehemu ambayo ina watoto Wanne wanaosoma uku wakiwa wanaishia kwenye Nyumba ya kupanga kutokana na Baba yao kuugua kwa zaidi ya Miaka 10 na hivyo kushindwa kufanya kazi.

  Dkt. Yonaz  amesema Mhe Makonda kwa kutambua mchango wa tasnia ya Habari hususani  waandishi wa Habari  amekubali kujenga Nyumba hiyo kama kielelezo cha Kumuenzi  Marehemu Athumani  ambae katika Uhai wake alikuwa Mpiga Picha Mahiri wa Magazeti ya Serikali nchini.

  Hatua hii imepokelewa kwa Furaha na baadhi ya waandishi wa Habari ambao wamesema Kitendo cha Makonda kukubali Kuijengea  Nyumba Familia ya Marehemu Athumani mbali na kuwafuta Machozi ya Huzuni, Bali kimekuwa ni fundisho Tosha kwa Baadhi ya waandishi ambao walikuwa Wakimchukia  Mhe Paul Makonda pasipo sababu za Msingi, na kukifananisha Kitendo hiki na Ukamilifu wa Maandiko katika vitababu vitakatifu yanayotutaka  TUWAPENDE ADUI ZETU.


Hakuna maoni: