Wakazi wa kijiji cha Mtegu Wilayani Tandahimba mkoani Mtwara, wamelalamikia serikali kwa kutowezesha kutumika kwa majengo ya zahanati waliyojenga kwa nguvu zao na michango yao.
Zahanati hiyo ambayo imeshakamilika majengo yake ilijengwa na wananchi hao kwa kujichangisha wenyewe fedha zao za korosho, ambapo kila mwananchi alikatwa shilingi 50 kwenye kila kilo moja ya korosho, lakini mpaka sasa hayatumiki na kulazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.
“Kama huna hela unakufa kabla hujapata huduma, sisi tunapata usumbufu sana, hatuoni kama hili jengo litaendelea, mpaka sasa hivi tunaoana vitu vya ajabu, sijui serikali ina mpango gani, tushachoka na hili”, amesikika mmoja ya wakazi hao.
Mkazi mwingine aliendelea kwa kueleza kwamba ...Uongozi wa Taifa na wilaya walikuja hapa wameona wakasema jengo ni kubwa hilo ni kituo cha afya, lakini mpaka sasa hakuna linaloendelea”, amesema mkazi huyo.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tandahimba Bw. Abdala Mfinanga, amekiri kutelekezwa kwa majengo hayo bila kufanyiwa kusudio husika, na kutoa sababu za serikali kutoanza kulitumia na kutoa huduma kwa wananchi.
“Sababu kubwa ya kutofunguliwa ni mapato, tatizo lingine kubwa hata zahanati zingine zilizopo hazina watumishi, lakini muda mfupi ujao itakuwa imekamilika, hata hivyo bado kuna vitu muhimu vya kuwekwa, kituo cha afya ni wahudumu na vifaa, wawe wavumilivu katika kipindi hiki cha mpito, hatuwezi kufungua zahanati hakuna watumishi”, amesema Bwana Mfinanga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni