Ijumaa, 13 Oktoba 2017

PICHA: KINACHOENDELEA VISIWANI ZANZIBAR KABLA YA KESHO OKTOBA 14

Wakati kesho Oktoba 14, ikiwa ni kilele cha Maadhimisho ya mbio za mwenge kitaifa ikiambatana na ibada ya misa maalumu ya kumbukumbu ya miaka 18 ya kifo cha Hayati Mwl Julius Nyerere  visiwani Zanzibar katika mkoa wa mjini magharibi.

Tayari wameanza kuripoti baadhi ya viongozi wa mikoa na wa kitaifa visiwani humo, ambapo Jana aliwasili Rais Wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, na leo Amewasili Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasan akiambatana na Baadhi ya viongozi wengine.


Mama samia amepokelewa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mahamoud pamoja na Mawaziri kutoka Tanzania Bara na wengine kutoka katika serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiongozana na baadhi ya mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Maandalizi ya sherehe hizo yameshakamilika katika Uwanja wa Amani uliopo Kisiwani Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi ambapo mgeni rasmi atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar na mwenyikiti wa Baraza la Mapindizu Dkt Ali Mohamed Shein. Hizi ni picha za maandalizi ya uwanja huo ulivyo kwa sasa.













Hakuna maoni: