Na Shaban Khamis,Morogoro
Chama cha wanafunzi wa Kiswahili Afrika Mashariki tawi la Chuo kikuu cha waislamu Morogoro (CHAWAKAMA-CHUKIWAMO) kimeadhimisha sherehe ya kumbukizi ya Nguli wa Mashairi Marehemu Shaaban Robert.
Sherehe hizo zimefanyika leo Januari Mosi, 2018 katika chuo kikuu cha waislamu Morogoror eneo la ukumbi mpya wa mikutano (NAH) ambapo mgeni rasmi alikuwa Prof.Joshua Madhumulia ,Makamu mkuu wa chuo Iringa. Pia kulikuwa na wageni wengine kutoka vyuo vya Jordan na UDSM.
Katika hotuba yake Prof.Joshua amesema ni vyema tukatumia Lugha ya Kiswahili vizuri ili tuweze kufika mbali kama kauli mbiu ya sherehe hiyo ilivyoasema kiswahili chetu ni urithi wetu kutoka kwa mababu zetu.

Prof.Joshua Madumulla
Katika sherehe hizo kumefanyika matukio mbalimbali yakiwemo kughani mashairi na kucheza igizo.
Shaabana Robert alizaliwa mwaka 1922 mkoani Tanga na alifariki mwaka 1962.Katika maisha yake Shaaban Robert aliandika vitambu mabalimbali maarufu vikiwemo
-Kusadikika,Nchi iliyo angani
-Maisha Yangu
-Kufikirika
-Adili na nduguze
-Wasifuwa siti Bint saad
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni