Jumatatu, 8 Januari 2018

APIGWA SHOTI YA UMEME NA KUFA HAPOHAPO WAKATI AKIANIKA NGUO KWENYE WAYA WA UMEME


Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Rahimu Haruni (30) mkazi wa mtaa wa Mwembesongo manispaa ya Morogoro amefariki dunia baada ya kupigwa na shoti ya umeme wakati akianika nguo kwenye waya uliofungwa kwenye nyumba inasadikika kuwa na hitilafu kwenye mfumo wa umeme.

Wananchi walitupia lawama shirika la umeme TANESCO mkoa wa Morogoro kushindwa kutatua tatizo hilo licha ya kudai kutoa taarifa ofisi za TANESCO bila mafanikio.

Tumeeshuhudia mwili wa kijana huyo ukiwa ulelala chini huku mafundi wa TANESCO wakizima umeme na kuanza uchunguzi wa tatizo hilo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi kwa kuhofia wananchi kujichukulia sheria mkononi.


Hakuna maoni: