Jumamosi, 30 Desemba 2017

YALIYIKUTWA KWENYE UKAGUZI WA MALI ZA CCM MTWARA

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mtwara, Yusuph Nannila ameanza zoezi la kufuatilia na kuhakiki mali za chama hicho kabla ya kamati aliyoiunda President JPM kufika katika mkoa huo.

Akiongozana na Kamati ya siasa ya Mkoa wa Mtwara Yusuph Nannila ameelezea vitu alivyobaini katika ziara ya yake ya jana December 29, 2017 katika kuhakiki mali za CCM.

“Moja ya vitu nilivyobaini watu hawana mikataba ya kukaa katika maeneo ya CCM, watu wameuziana mali za chama, kwa hiyo ni kweli kwamba watu wengi wameuziana mali za CCM na chama kinaonekana hakina uwezo,” – Mwenyekiti CCM Mtwara



Hakuna maoni: