Jack Wilshere na Theo Walcott wanatumai kwamba meneja wa Arsenal Arsene Wenger atafurahishwa kiasi cha kuwatumia kwenye mechi baada yao kucheza vyema sana Alhamisi.
Walicheza vizuri sana mechi ya Europa League ambayo walishinda kwa mabao mengi dhidi ya Bate Borisov.
Wawili hao hawajapewa nafasi ya kucheza kikosi cha kuanza mechi Arsenal katika Ligi ya Premia msimu huu, lakini wote wawili walitikisa wavu na kusaidia Arsenal kulaza Bate Borisov 6-0 na kumaliza mechi za Kundi H kwa ushindi.
"Kuna ushindani mkali unapokuwa unachezea Arsenal. Tufanya kadiri ya uwezo wetu kumfanya meneja ajikune kichwa akijaribu kuchagua wachezaji wa kutumia," Walcott amesema.
Wenger alifanya mabadiliko 11 kwenye kikosi chake kilicholazwa na United kwa mechi hiyo ya Alhamisi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni