Jumapili, 10 Desemba 2017

Video ya Babu Seya yampiku Diamond kwa kuangaliwa zaidi

Siku moja baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli kutangaza msamaha wa kumwachia huru Mkongwe wa Muziki wa Dansi nchini Nguza Viking 'Babu Seya'  na mtoto wake Johnson Nguza 'Papii Kocha' video yao wakionekana wanatoka gerezani imeshika namba moja kwa kuangaliwa zaidi na watu wengi katika mtandao wa Youtube na hivyo kuishusha video mpya ya Diamond.

Video ya wimbo mpya wa Diamond aliomshirikisha mkali kutoka Marekani, Rick Ross unaokwenda kwa jina la Waka ulikuwa ukikamata nafasi ya kwanza lakini tangu Mtandao wa Muungwana Blog kuiweka video ya Seya na Papii wakitoka gerezani imejikuta ikifunika video zote.

Babu Seya na mwanae Papii Kocha ni miongoni mwa wafungwa zaidi ya 8000 waliopata msamaha wa Rais Magufuli jana katika sikukuu ya Uhuru ikiwa ni baada ya kukaa gerezani kwa takribani miaka 14 ambapo walikuwa wakitumikia kifungo cha maisha jela.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USISAHAU KUSUBSCRIBE






Hakuna maoni: