Jumamosi, 16 Desemba 2017

TUNDU LISSU AMJIBU VIKALI SPIKA NDUGAI

Amesema kuwa watu walioleta Nairobi ni pamoja na Spika wa bunge na uongozi wote wa bunge, na kusema ndege hiyo inamaanisha ndege iliruhusiwa na serikali ya Tanzania, na spika au Serikali asilete hoja kuwa sehemu aliyopelekwa ndio inakuwa kikwazo yeye kulipiwa gharama kama anavyostahili kulipiwa mbunge yeyote na Serikali.

Ameelezea kuwa haijawahi kutokea katika historia ya Tanzania mbunge kuuawa akiwa kazini, na matendo yaliyotokea baada ya yeye kushambuliwa yanatia wasiwasi.

CCTV camera zimeondolewa, polisi hawajampata mshukiwa hata mmoja na pia wamepiga marufuku watu kumuombea, kujitolea damu, kuvaa t shirt zenye jina lake, yaani ni kama wamepiga marufuku jina la Tundu Lissu

Hivyo hii inaonyesha polisi hawawezi kuwa huru katika upelelezi wa kumpata aliyemshambulia na wanahitaji kuleta wapelelezi kutoka nje

Ametolea mfano Kenya waziri wa mambo ya mambo ya nje Robert Ouko aliuawa mwaka 1993 watu waliishuku Serikali kuhusika, na Serikali ikaleta wapelelezi kutoka nje,pia kuna wakati benki kuu iliungua.

Pia benki kuu yetu ilipoungua moto miaka ya 1980s walileta wachunguzi kutoka nje, hivyo sio ajabu kuomba msaada kutoka nje

Amesema tukiola kushambuliwa kwake ni ugaidi, unapomshambulia mtu kwa lengo la kumuu kwa sababu za kisiasa huo unaitwa ni ugaidi



Hakuna maoni: