Mkuu wa jeshi la polisi nchini(IGP) Simoni Sirro, amesema tuhuma zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani kuwa polisi walihusika kuwatoa nje wasimamizi wa uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika hivi karibuni si za kweli kwa sababu hajawahi kupokea barua ama malalamiko ndani ya ofisi yake kutoka kwa viongozi hao.
IGP Sirro ameyasema hayo mkoani Lindi, wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kwamba tuhuma hizo zinazotolewa na viongozi hao si za kweli kwani hajawai kupata malalamiko hayo na kusema kuwa kama kuna mtu ana ushahidi na tukio hilo atoe taarifa mara moja ndani ya jeshi la polisi ili waweze kupeleleza na kuchukua hatua.
Hata hivyo IGP Sirro akasema jeshi la polisi nchini limejipanga katika kuhimarisha ulinzi katika sikukuu zote mbili za Noeli na mwaka mpya .
Aidha IGP Sirro mara baada ya kufika mkoani Lindi aliweza kukutana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na pia akatembelea kambi ya kisosi ya kutuliza ghasia aliweza kuangalia mazoezi mbalimbali yanayofanya na jeshi la polisi mkoani Lindi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni