Mbunge wa Jimbo la Mikumi kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Haule maarufu kwa jina la Profesa Jay, imedaiwa kuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi la Mkoa wa Morogoro, wanatafutwa yeye pamoja na baba yake mzee Steven Haule.
RPC Morogoro, Urichi Matei amethibitisha kumtafuta Joseph Haule na baba yake mzee Steven Haule kwa madai ya kukutwa kwa matrekta ambayo ni mali ya SUMA JKT yakiwa nyumbani kwa mzee Steven Haule.
Matrekta hayo yanaripotiwa kuwa walinyang’anywa madereva na kudaiwa yanarudishwa SUMA JKT ambao ndiyo wamiliki kwani bado yanadaiwa hayajamaliziwa mkopo ila baadaye yakakutwa nyumbani kwa mzee Steven Haule.
“Hizi trekta zimekutwa nyumbani kwa mzee Steven Haule ambaye ni baba yake na huyu mbunge Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay, zimefika pale kwa namna gani hatujui ila kwa sasa hivi nimemuelekeza OCD kumtafuta bwana Steven Haule na Joseph Haule ili watusaidie zile trekta kama ni mali yao au wamezipataje” alisema RPC Urichi Matei.
Kwa mujibu wa kituo cha Channel Ten alipopigiwa simu Profesa Jay alieleza kuwa matrekta hayo yameifadhiwa kwa muda mahala penye usalama kwa ajili ya kurudishwa SUMA JKT na siyo vinginevyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni