Mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 na 12 ambayo ilizinduliwa mapema wiki hii katika Uwanja wa Nyamagana, Mwanza na Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza James Bwire na kushuhudia michezo takriban 10, inaendelea kushika kasi.
Akizungumza na ShutiKali, katibu mkuu wa Chama cha Soka Wilaya ya Nyamagana, Gilbert Dady amesema katika michuano hiyo kuna timu 16 ambazo 8 ni za umri chini ya miaka 15 (U15) na nane ni za U12.
Timu shiriki ni Marsh Athletics, TSC Academy pamoja Sports Center, Ncheye Sports, Nyahingi, Mahina Youth, AC Youth, Rwegasore Kids, Issa Sports Center, Corner Youth, Zully Sports, Mwanza City, Maduka Youth, Coop Youth, Young Boys, Kilimo FC na Mahina Youth.
“Lengo la mashindano haya ni kuhakikisha tunapata vijana wenye uwezo wa kucheza mpira na kuhakikisha tunawalea katika misingi ya soka na kufanikisha tunakua na timu bora ya Mkoa ya Vijana itakayoiwakilisha Mwanza katika Mashindano ya Vijana,” alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni