Jumamosi, 16 Desemba 2017

MTOTO NJITI, AINA ZAKE NA SABABU HATARISHI ZINAZOFANYA MAMA AZAE MTOTO NJITI




Njiti ni kitendo cha mtoto kuzaliwa mapema au kwa lugha ya kitaalamu huitwa, Premature birth, hutokea pale ambapo mtoto anazaliwa kabla ya kufikisha wiki 37 (kabla hajafikisha miezi tisa akiwa tumboni mwa mama yake)

Mama mjamzito anapozaa mtoto kabla ya wakati wake, huyo mtoto huitwa Njiti (premature baby), anakuwa bado ajafikisha mda Wake wakuzaliwa na mwili Wake unakuwa bado haujakomaa.


Aina za watoto njiti

watoto njiti wanakuwa wanatofutiana umri

- kunawale wanao zaliwa wakiwa na umri wa chini ya wiki 28

-kuna wanaozaliwa wakiwa na wiki 28 -32

-kundi la mwisho wanakuwa wanazaliwa wakiwa na wiki 32-37.


Namna ya kuwahifadhi watoto njiti (premature babies)
Hii hutegemea na umri wa wiki aliozaliwa nao mtoto

-Watoto njiti huwa wanahifadhiwa kwenye kifaa maalum kinaitwa (incubator) kinachowapa joto la kutosha kama alilokuwa analipata akiwa ndani ya tumbo la mama yake

-Njia nyingine inaitwa Kangaroo mother care mtoto anawewa kifuani kwa mama yake (skin to skin contact) akiwa hana nguo ila atavarishwa soksi na kofia na atafunikwa ili apate joto la kutosha ni njia moja wapo ya kumpa mtoto ambaye ni njiti joto.


Sababu hatarishi zinazopelekea mama azae mtoto njiti (premature baby

-Kushika mimba ukiwa na umri chini ya miaka 17 na ukiwa na miaka 35 au zaidi unakuwa kwenye hatari ya kuzaa mtoto njiti

-Unywaji wa pombe katika kipindi cha ujauzito

-Upungufu wa damu mwilini.

-Uzito mkubwa kwa mama kipindi cha ujauzito au kuwa na uzito mdogo sana

-Uvutaji wa sigara(tumbaku) au bangi na utumiaji wa madawa ya kulevya

-Magonjwa sugu kama kisukari, shinikizo la damu la juu

-Kifafa cha mimba

-Maambukizi katika via vya uzazi na njia ya mkojo

-Mama akiwa na matatizo kwenye mfuko wa uzazi(uterus) na shingo ya kizazi (cervix)

-Mama kushika mimba haraka baada ya kujifungua (miezi sita baada ya kujifungua)

-Mama anapokuwa na mimba ya mapacha(twins) anakuwa na hatari ya kuzaa mtoto njiti

-Mama kuwa na msongo wa mawazo kunaweza mfanya azae mtoto njiti

-Mama mjamzito kuwa na lishe duni ni sababu mojawapo ya kuweza kuzaa mtoto njiti.
Read more »

Hakuna maoni: