Jumamosi, 16 Desemba 2017

DALILI ZA MAMA MJAMZITO ANAYEWEZA KUZAA NJITI,NAMNA YA KUJIKINGA KUZAA NJITI



Dalili za mama mjamzito anayeweza kuzaa mtoto njiti

 ukishaziona Dalili zifuatazo  inatakiwa uwahi hospitali haraka iwezekanavyo

-Maumivu ya mgongo-utasikia mgongo unauma sana maeneo ya chini maumivu yakuja na kuondoka .

-Maumivu ukeni kunavuta na kuachia kila baada ya dakika 10.

-Kutokwa maji maji ukeni kwa wingi.

-Kutokwa damu inaweza kuwa nyingi au kidogo ukeni

-kuhara,kutapika

-Maumivu chini ya kitovu yaani maumivu ya uchungu

-Mtoto kukusukuma kuja chini.(utahisi msukumo mkubwa kuja chini)



Matatizo  wanayopata watoto njiti (premature babies) baada ya kuzaliwa

Baadhi ya watoto njiti wanakuwa na changamoto mbali mbali za kiafya ikiwemo

-Matatizo katika neva za fahamu

-Matatizo kwenye ubongo

 -Matatizo katika mfumo wa upumuaji (mapafu kushindwa kutanuka na kusinyaa wakati wa upumuaji kutokana na kukosekana kwa protini maalumu (surfactant) katika mapafu),

-kupata matatizo ya damu

-kupata homa ya manjano kutokana na Ini kutokukomaa vizuri,

-Matatizo katika uwezo wa kuona pamoja

-Kuwa na hatari ya kupata magonjwa ya kuambukizwa kwa kirahisi.



Namna ya kuweza kujikinga ili kutozaa mtoto njiti (premature baby)

Ingawa hakuna sababu ya moja kwamoja inayosababisha mama kuzaa mtoto njiti (premature baby), lakini Inatakiwa tujikinge na tabia hatarishi zinazopelekea tatizo hili la wakina mama kujifungua watoto njiti kama ifuatavyo

-Kula vyakula bora hata kabla ya kutarajia kupata ujauzito

-Kuacha Unywaji wa pombe,uvutaji wa sigara na matumizi ya madawa ya kulevya

-Kuanza kliniki mapema kwa mama mjamzito ili oupewa elimu juu ya kulea mimba na  kuweza kufanyiwa uchunguzi na kupimwa vipimo muhimu

-Mama mjamzito kulala ndani ya chandarua chenye dawa  ili kujikinga na ugonjwa wa malaria.


Hakuna maoni: