Alhamisi, 28 Desemba 2017

Mti wa kihistoria katika Ikulu ya Marekani kukatwa

Washington, Marekani. Mti ulipandwa takriban miaka 200 iliyopita katika Ikulu ya Marekani unatarajiwa kukatwa.

Mti huo aina ya Magnolia una maua yenye kung’aa na yanayonukia.

Ulipandwa miaka ya 1800 na Rais Andrew Jackson baada ya kifo cha mkewe.

Tangu ulipopandwa umekuwa kivutio kwa wengi lakini utakatwa kutokana na kuhatarisha usalama.

Wataalamu wanasema mti huo umeharibika hivyo kuwa hatari kwa usalama katika eneo la Ikulu.

Melania, mke wa Rais Donald Trump ametaka sehemu kubwa ya mti huo kuondolewa baada ya kuwasiliana na wataalamu.

Amesema uamuzi huo unatokana na mti huo kuhatarisha usalama wa wageni wakiwemo waandishi wa habari ambao mara zote husimama mbele yake wakati helikopta ya Rais inapokaribia kuruka.

Msemaji wa Ikulu ya White, Stephanie Grisham amesema Melania ametaka masalia ya mti huo yaachwe ili kuoteshwa katika eneo hilo.

Hakuna maoni: