Jumamosi, 23 Desemba 2017

Jafo apongeza miundombinu Ubungo

Manispaa ya Ubungo imepongezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Suleiman Jafo, kwa kujenga shule ya Sekondari ya Mavulunza iliyoko Kimara jijini Dar yenye madarasa manane kwa fedha zake za ndani ambapo shule hiyo inatarajiwa kuzinduliwa mwaka kesho Januari.

“Napongeza juhudi zilizofanywa na manispaa ya Ubungo kwa kujenga shule hii na vyoo lakini mahali hapa palipojengwa si salama kutokana na miundombinu ya hapa kuwa ya bondeni, kwa hiyo nawaomba idara zote zinazohusika mtafute eneo jingine ndani ya miaka mitatu mjenge sehemu shule nyingine,” amesema Jafo.

Vilevile, akiwa katika kituo cha afya cha Kimara, Jafo amezunguza na wananchi waliofika kutibiwa na kuwaeleza kwamba serikali ina mpango wa kujenga jengo la ghorofa ili kupanua huduma za afya katika wilaya ya Ubungo.

Alimwagiza pia mhandisi wa manispaa hiyo kutumia vizuri fedha zaidi ya Sh. bilioni nne zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa zahanati hiyo.

Hakuna maoni: