Jumapili, 31 Desemba 2017

DR.SHIKA AKATAA DILI ZA MATANGAZO KUHOFIA ATAFUATILIWA

Mtanzania Dkt. Louis Shika aliyejizolea umaarufu mkubwa hivi karibuni katika mitandao na vyombo vya habari ameeleza sababu ya kuacha kufanya matangazo ya kibiashara na kampuni mbali mbali.

Umaarufu wa Dkt. Shika ulikuja baada ya kujitokeza katika mnada wa  kuuza nyumba za Lugumi ambapo aliahidi kununua nyumba hizo kwa thamani ya Sh bilioni 2.3 lakini alishindwa kulipia asilimia 25 ya fedha hizo ambazo ni shilingi milioni 800, kisha kudai anangojea fedha zake kutoka nchini Urusi.

Dkt. Shika amekiambia kipindi cha Weekend Breakfast cha EA Radio kuwa ameacha kufanya matangazo kwa kuhofiwa kufuatiliwa na maadui zake kutoka nchi ya Urusi alipokuwa akifanya kazi miaka ya nyuma.

“Sina interest na haya matangazo tena kwa sababu wale Warusi niliowakimbia watani-track watajua niko wapi, lakini natoa ushirikiano kwa wenzangu huku nikiwa nimetafuta means nyingine za kuwakwepa,” amesema Dkt. Shika.

Dkt. Shika ameweza kufanya tangazo la kampuni moja ya michezo ya ubashiri matokeo katika soka, pia ameweza kuonekana katika video mbili za nyimbo za Bongo Flava. Video hizo ni za Kundi la Rostam ‘Kiba_100’ na wimbo wa Gaza ‘Nanii’ akishirikiana na Madee.



Hakuna maoni: