Jumatano, 22 Novemba 2017

YANGA WAKIFUATA UTARATIBU HUU,WATAFANIKIWA KUMSAJILI MO IBRAHIM


Baada ya dirisha dogo la usajili Tanzania bara kufunguliwa  15 Novemba ,2017 kuna tetesi mbalimbali zimeibuka za wachezaji kusajiliwa na vilabu mbalimbali.

Moja ya tetesi kubwa ni ile ya Mchezaji wa Simba Mo Ibrahim kusjiliwa na Klabu ya Yanga. 


Mratibu wa Klabu ya Simba Abbas suleimani ameibuka kulitolea ufafanuzi suala hilo kwa kusema licha ya Mo Ibrahim bado ni mchezaji wa Simba mwenye mkataba, ila kama mambo yatafuata utaratibu na uongozi pamoja na benchi la ufundi likawa tayari kumwachia, basi mchezaji huyo anaweza kutua Jangwani.

Abbas ameyasema hayo wakati akihojiwa na kituo cha radio cha  Dream Fm cha jijini Mbeya

"Offcourse tetesi zipo lakini sisi kama taasisi tumejipangia utaratibu  wa kufanya kazi,hatufanyii kazi tetesi."

Tukisema tufanyie kazi tetesi wakati Mo ni mchezaji halali wa Simba na tunajua mkataba wake unafahamika, lakini Yanga kama wanamhitaji Mo kuna taratibu ambazo wanaweza kuzifuata wakaweka mezani. Viongozi wa Simba ni wasikivu wanaweza kuangalia umuhimu wa Mo, wanaweza wakaangalia kiwango cha Mo na wakafikia makubaliano" ,Abbas Suleiman


Hakuna maoni: