Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameendelea kusisitiza kuwa wananchi hawapaswi kununua damu kwani huduma hiyo ni bure kwa watanzania wote katika hospitali zote.
Hayo amezungumza leo jijini Dar es salaam, wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait katika Taasisi ya Mifupa MOI ambapo ulihuzuriwa na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania.
“Watanzania wanaohitaji huduma ya kuongezewa damu wapewe bure marufuku kwa watoa huduma za vituo vya afya pamoja na hospitali zote kuuza damu hiyo kwani inatoka kwa wananchi wenyewe” alisisitiza Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa wananchi wanatakiwa kujitokeza katika kuchangia damu ili kuweza kuwa na hifadhi ya kutosha na kufanya kazi kwa wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo kwa wakati sahihi bila ya usumbufu wowote katika kuokoa maisha ya watanzania.
Mbali na hayo Waziri Ummy ameongeza kwamba kuanzia mwakani 2018 Tanzania itaanza kutoa huduma ya matibabu ya kupandikiza figo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni