Ijumaa, 17 Novemba 2017

Watanzania waombwa kuchangia Miguu Bandia

Hospitali ya CCBRT imeguswa na Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda ya kutafuta Miguu Bandia kwa watu wenye uhitaji kwa kuwapatia matibabu Wagonjwa 35 waliokatwa Miguu kutokana na Ugonjwa wa kisukari.

Miguu hiyo ya kisasa ina thamani ya zaidi ya Shilling Million 157 ambapo Kati ya  Wagonjwa 35 waliokuwa wakitembelea Magongo kwa muda mrefu baada ya kukatwa miguu, 21 wameshawekewa Miguu Bandia na sasa wanaendelea na Shuguli zao baada ya kuwa wazima.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam Mheshimiwa Makonda amewashukuru watu wote ambao wamechangia na wanaoendelea kuchangia kwani msaada wao wasione kama watupa, wenye uhitaji wa miguu bandia ni wengi hivyo amewaomba watanzania kuendelea  kusaidia.

Hakuna maoni: