Jumamosi, 25 Novemba 2017

TANZANIA INA UPUNGUFU WA WATUMISHI WA AFYA 95,059-JPM




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa serikali inatambua uhaba wa watumishi wa afya wapatao 95,059 hivyo serikali imetoa vibali vya ajira zipatazo 3410.

“Pamoja na kwamba kuna mambo ya afya yanatia moyo lakini pia natambua kama sekta yetu ya afya tuna kabiliwa na matatizo kadhaa moja ya matatizo hayo ni uhaba wa watumishi wa afya na tatizo hili kimsingi lina sura kuu mbili, sura ya kwanza ni uhaba wa watumishi wenyewe nchi yetu bado ina matatizo makubwa ya watumishi wa afya 89,842,” amesema Rais Magufuli. 

“Hivyo tuna upungufu wa watumishi wa afya takribani 95,059 serikali ina lifahamu hili na ndio maana imetoa vibali vya ajira zipatazo 3410 na katika humo kutakuwa na madaktari na wataalam mbalimbali lengo ni kupunguza pengo la watumishi wa afya lililopo.”


Hakuna maoni: