Kiungo wa Simba Said Ndemla aliyekwenda nchini Sweeden kujaribu kucheza soka la kulipwa nchini humo amefanikiwa kupita katika majaribio hayo hivyo atarejea Nchini kukamilisha taratibu za makubaliano baina ya klabu ya simba na Eskilstuma ya huko Sweeden.
Ndemla ambaye kwa kipindi kirefu amekua akihusishwa na taarifa za kujiunga na klabu tofauti za hapa Nchini zikiwemo Azam na Yanga anatarajiwa kuwasili jumatano hii kujiunga na wenzake kuendelea na mzunguko wa ligi kuu kwa muda.
Hii hapa ndiyo taarifa ya Simba:
Simba Sports Club
Dar es salaam
25-11-2017.
TAARIFA KWA UMMA
_____________________________
Mchezaji Said Hamis Juma (Ndemla) amefanikiwa kufuzu kwenye majaribio yake ya kucheza Soka la kulipwa barani Ulaya.
Ndemla aliyekuwa nchini Sweden kwa majaribio kwenye klabu ya Eskilstuna ya huko.anatarajiwa kurejea nchini siku ya jumatatu inayokuja.
Na mara baada ya kurejea. klabu za Simba na Eskilstuna zitaanza mazungumzo ya kimkataba ili kumwezesha kiungo huyo kwenda Sweden kwa ajili ya kucheza Soka huko.
Kiufupi klabu imefurahishwa na azma ya Ndemla ya kutaka kusonga mbele zaidi, na kama ilivyo desturi na utamaduni wa Simba, klabu haitasita kumruhusu mchezaji yoyote anayepata fursa adhimu kama hiyo itakayomsaidia mchezaji binafsi.klabu na Taifa kwa ujumla.
Wakati huo huo kesho klabu ya Simba itakutana na viongozi wote wa matawi.
Mkutano huo ni maandalizi ya mkutano mkuu maalum wa klabu wa tarehe 3-12-2017. na mkutano huo wa kesho utafanyika makao makuu ya klabu kuanzia saa Nne kamili asubuhi ya jumapili ya tarehe 26-11-2017.
Mwisho
Uongozi wenu unawaomba Wanachama na washabiki wa klabu yetu kujitokeza kwa wingi kesho uwanja wa Uhuru kuishangilia timu yao, itakapocheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Timu ya Lipuli ya Iringa.
Imetolewa na.....
HAJI S. MANARA
Mkuu wa Habari na mawasiliano Simba Sports Club.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni